31-Hadiyth Al-Qudsiy: Mashuhadaa Wako Hai Jannah Wanatamani Kurudi Duniani Kupigana Tena Fiy SabiliLLaah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 31 

Mashuhadaa Wako Hai Jannah Wanatamani Kurudi Duniani

Kupigana Tena Fiy SabiliLLaah

 

عَنْ مَسْرُوقٍ قَالَ سَأَلْنَا عَبْدَ اللَّهِ عَنْ هَذِهِ الْآيَةِ:  ((وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ))  قَالَ أَمَا إِنَّا قَدْ سَأَلْنَا عَنْ ذَلِكَ فَقَالَ:  ((أَرْوَاحُهُمْ فِي جَوْفِ طَيْرٍ خُضْرٍ لَهَا قَنَادِيلُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ تَسْرَحُ مِنْ الْجَنَّةِ حَيْثُ شَاءَتْ ثُمَّ تَأْوِي إِلَى تِلْكَ الْقَنَادِيلِ فَاطَّلَعَ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ اطِّلَاعَةً فَقَالَ: هَلْ تَشْتَهُونَ شَيْئًا؟  قَالُوا: أَيَّ شَيْءٍ نَشْتَهِي وَنَحْنُ نَسْرَحُ مِنْ الْجَنَّةِ حَيْثُ شِئْنَا؟ فَفَعَلَ ذَلِكَ بِهِمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ،  فَلَمَّا رَأَوْا أَنَّهُمْ لَنْ يُتْرَكُوا مِنْ أَنْ يُسْأَلُوا قَالُوا: يَا رَبِّ! نُرِيدُ أَنْ تَرُدَّ أَرْوَاحَنَا فِي أَجْسَادِنَا حَتَّى نُقْتَلَ فِي سَبِيلِكَ مَرَّةً أُخْرَى،  فَلَمَّا رَأَى أَنْ لَيْسَ لَهُمْ حَاجَةٌ تُرِكُوا)) مسلم،  الترمذي، النسائي وابن ماجه

Masruwq (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Tulimuuliza ‘Abdullaah kuhusu Aayah: ((Wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa)) [Aal-‘Imraan 3: 169] Akasema: Ama tuliuliza kuhusu Aayah hiyo akasema: (Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Roho zao zimo ndani ya ndege wa kijani wenye kandili zinazoning’inia kutoka kwenye ‘Arsh wanatembea Jannah huria popote wapendapo, tena hujibanza kwenye hizo kandili. Rabb wao Aliwatupia jicho na Akasema: Je, Mnataka chochote? Wakasema: Tutake nini tena na tunajifaragua tutakavyo Jannah? Alifanya hivyo (Rabb) mara tatu. Walipoona hawataachiwa kuulizwa (tena) walisema: Yaa Rabb! Tungependa roho zetu Uzirejeshe katika viwiliwili vyetu ili tuweze tena kupigana kwa ajili Yako. Tena (Rabb) Alipoona hawahitaji chochote waliachiwa)) [Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

Share