Utulivu Wa Nafsi (Sakiynatun-Nafs) - 3

Utulivu Wa Nafsi (Sakynatun – Nafs) – 3

 

Imekusanywa na Ukht Haliymah’ Abdullaah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

7. Muumin Anaishi Pamoja Na Urafiki (Suhba) Ya Manabii Na Wakweli 

 

 

Muumin hahisi kwamba ametengeka na nduguze Waumini, hakika wao ikiwa hawapo naye Msikitini au nyumbani kwake daima wanaishi katika dhamira yake. Akiswali hata akiwa peke yake anaongea kwa jina lao. Kauli Yake Allaah (‘Azza wa Jalla):    

 إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

“Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” [Al-Faatihah: 5]

  

Akiomba du’aa anaomba kwa jina lao (tuongoze njia iliyonyooka), akijikumbuka nafsi yake anawakumbuka (amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah).

 

Muumin haishi na nduguze Waumini wa wakati wake tu bali anaishi na Waumini wa karne zote hata ikiwa imepita baina yao miaka anasema waliyosema watu wema katika Kauli ya Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا ﴿١٠﴾

“Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini;” [Al-Hashr: 10]

 

Muumin anahisi anaishi kwa imani yake na matendo yake mema pamoja na Manabii wa Allaah na Rusuli Wake. Na pamoja na kila mkweli, shahiyd, mtu mwema katika kila ummah na kila zama:

 

Anasema Allaah (‘Azza wa Jalla): 

 

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

“Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao.” [An-Nisaa: 69]

 

Ni nani ana furaha zaidi ya yule anayefungamana na hawa? Mafungamano haya si ya kimwili na sura tu bali ni mafungamano ya kiroho, kifikra na kimoyo.

 

 

 

8. Swalaah Na Du’aa Ni Vinavyopelekea Utulivu  

 

Katika sababu ya utulivu wa nafsi ambayo wamenyimwa wenye kuabudia mali wakaneemeshwa nayo Waumini wakawa wanaongea na Rabb wao kila siku katika Swalaah na du’aa …

 

Swalah ni fursa ya mtu kuisafisha nafsi yake na shughuli za kidunia asimame mbele ya Rabb wake kwa kumtukuza hali akimuomba. Katika kuwasiliana na Allaah (katika Swalaah) kunaipa nafsi nguvu na matumaini kwa roho nayo ni silaha ya Muumin anayoitumia katika vita vya kimaisha na kupambana na balaa zake na vyenye kutia uchungu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

  يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

“Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri.” [Al-Baqarah:153]

 

Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) likimtingisha jambo lolote anakimbilia Swalaah na haikuwa Swalaah yake ni picha tu bali ilikuwa ni katika kuwa faragha na kunong’ona na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), mpaka ikawa ikifika wakati wa Swalaah anamwambia muadhini wake Bilaal (Radhiwya Allaah ‘anhu):

 

“Tufurahishe kwayo ee Bilaal”

 

na alikuwa akisema:

 

“Nimejaaliwa kitulizo cha macho yangu katika Swalaah”.

 

Amesema Deen Carnegie katika kitabu chake ‘Acha yanayokutatiza na uanze maisha’:  “…Swalaah inakuhakikishia mambo matatu haijalishi uwe ni Muumin au Mulhid (anayeitoa kasoro dini na kutoiamini).

 

 

 i-Swalaah ni usaidizi katika kuelezea yanayoshughulisha nafsi yako na yaliyo mazito, wamebainisha wema waliopita kwamba haiwezekani kukabiliana na tatizo ambalo halijulikani, Swalaah ni sawa na kitabu ambayo anaelezea mwenye fani ya Adab (Adiyb)  matatizo yake (humuum), tukitaka suluhisho la matatizo yetu ni wajibu kwetu iwe wazi katika ndimi zetu na hivi ndivyo tunavyofanya tukimuelezea matatizo yetu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

 

ii-Swalaah inakufanya uhisi huko peke yako katika kutatua matatizo yako na yanayokuhuzunisha (humuum), mara nyingi matatizo yatukutayo ya kibinafsi tunashindwa kuwaelezea hata watu walio karibu yetu lakini kwa mapana tunamuelezea Allaah (‘Azza wa Jalla) katika Swalaah.

 

Madaktari wa nafsi wanakubaliana kwamba tiba ya maradhi ya kinafsi (Tawaatur Al-‘Aaswaab) kwa kuwaelezea marafiki wa karibu sana na ndugu mpenzi sababu ya matatizo uliyonayo, tusipopata wa kumueleza anatutosha Allaah kuwa msaidizi wetu.

 

 

iii-Swalaah ni hatua ya mwanzo kuiendea kazi. Inawezekana mtu akawa anaswali siku baada ya siku bila ya kupata faida yaani haiboreshi hali yake na kutatua yamkumbayo.

 

Ikiwa hii ni hali ya Swalaah kwa ujumla (kwa wasio Waislamu) basi Swalaah katika Uislamu ina athari zaidi ya hivi ndani yake kuna twahara inayochangamsha mwili, Qur-aan isomwayo nacho ni Kitabu cha kudumu, kuhuisha jama’ah ambayo imesisitiza na kuhimiza Uislam. Utulivu ulioje anaohisi Muumin pindi anapomwelekea Rabb wake wakati wa matatizo na siku ya shida anamuomba kama alivyoomba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

 

“Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arshi tukufu, Rabb wetu na Rabb wa kila kitu, Mwenye kuichanua tembe ya mbegu na kokwa, na Aliyeteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan, najikinga Kwako kutokana na shari ya kila kitu, Wewe Ndiye Mwenye kukamata utosi wake, Ee Allaah Wewe Ndiye wa Mwanzo, hakuna kabla Yako kitu, na Wewe Ndiye Uliye wazi, hakuna juu yako kitu chochote, na Wewe Ndiye Uliyefichika, hakuna kilichojificha chini Yako, tulipie madeni yetu, na utuepushe na ufakiri.” [Muslim]

 

Dokezo: Du’aa hii pia ni katika du’aa za kusoma wakati wa kulala usiku ipo katika kitabu kidogo cha du’aa ‘Hiswnul Muslim.’

 

Na ni ipi matumaini kama aliyoshushiwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) moyoni mwake alipokuwa anarudi kutoka Twaaif miguu miwili ikiwa inavuja damu, amejeruhiwa moyo kutokana na mabaya aliyokumbana nayo kwa watu hao, haikuwa kwake ila kunyanyua mikono yake mbinguni huku moyo wake ukiwa baridi na salama na kusema:

 

“Ee Allaah mimi nashtakia udhaifu wa moyo wangu na uchache wa hila yangu na kudharauliwa na watu. Ee Mwenye kurehemu mwingi wa Rahmah, Wewe Ndiye Rabb wa wenye kutiwa udhaifu (Mustadhw’afiyn), nawe Ndiye Rabb wangu…”

 

 

9. Muumin Haishi Baina Ya ‘Lau’ Na ‘Layta’

 

 

Sababu kubwa ya matatizo (Qalaq) ambayo anakosa mwanaadamu utulivu wa nafsi, amani, radhi ni kujutia wakati uliopita na kukasirikia wakati uliopo na khofu ya wakati ujao.

 

Baadhi ya watu inawashukia misiba anabaki nayo miezi na miaka anajikumbushia maumivu yake wakati mwengine akijuta na wakati mwengine akiwa na matumaini “laiti ningefanya, laiti ningeacha, lau ningefanya vile ingekuwa hivi.”

 

Madaktari wa nafsi wao pamoja na waelekezaji wa kijamii na watu wa malezi na kazi, wanatoa nasaha kwamba mwanaadamu asahau maumivu yaliyopita na aishi sanjari na wakati uliopo Kwani wakati uliopita haurudi.

 

Udhaifu wa mwanaadamu unawakumba wengi unawajaalia watwange unga uliokwishatwangwa wanalilia wakati uliopita wanang’ata vidole vyao kujutia yaliyopita. Muumin wa kweli amesalimika na hisia hizi Kwani anaamini Uwezo na makadirio ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) hajisalimishi nafsi yake kutokana na matukio yaliopita anaitakidi kwamba jambo Analotaka Allaah huwa.

 

Muumin anaelewa Alilokadiria Allaah huwa hivyo, kwanini akasirike?

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿٢٣﴾

“Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla hatujautokezesha. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi. Ili msisononeke juu ya yale yaliyokuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allaah); na Allaah Hapendi kila mwenye kujinata, anayejifakharisha.” [Al-Hadiyd: 22-23]

 

 Katika vita vya Uhud ambapo waliuawa Waislamu sabini, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Alielezea hali za wanafiki wenye maradhi ya moyo na madhaifu wa imani walioishi baina ya ‘lau’ na kujutia kwa kusema ‘layta’ laiti..

 

 وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

“Kundi miongoni mwenu na kundi likawashughulisha nafsi zao wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili; wanasema: Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili? Sema: Hakika amri yote ni ya Allaah. Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa. Sema: Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuawa kwenye mahali pa kuangukia wafe. Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani.” [Al-‘Imraan: 154]

 

Akawarudi (Allaah) hao waliowaambia Ndugu zao hali wao hawakwenda:

 

الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٦٨﴾

“Wale waliowaambia ndugu zao nao wakakaa (wasiende vitani): Lau wangelitutii basi wasingeliuawa. Sema: Basi ziondoleeni nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli.” [Al-‘Imraan: 168]

  

Muumin hawi kama hawa wanafiki wala Ndugu zake makafiri ambao Qur-aan imekataza kujifananisha nao katika kujuta kwao na matamanio yao ya kihuzuni.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَّوْ كَانُوا عِندَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١٥٦﴾ وَلَئِن قُتِلْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوْ مُتُّمْ لَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَحْمَةٌ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ﴿١٥٧﴾

“Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kwa ndugu zao; waliposafiri katika ardhi au walipokuwa vitani: Lau wangelikuwa kwetu wasingelikufa na wala wasingeliuawa, ili Allaah Afanye hayo (yaliyoeleweka vibaya) majuto katika nyoyo zao. Na Allaah Anahuisha na Anafisha. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye kuona. Na kama mtauliwa katika njia ya Allaah au mtakufa; bila shaka maghfirah kutoka kwa Allaah na rahmah ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.” [Al -‘Imraan: 156-157]

 

Alama (shi’aar) ya Muumin daima ni kusema “Amekadiria Allaah na Analotaka huwa, Namshukuru Allaah kwa kila hali”. Na kwa hilo hatajutia yaliyopita wala haishi kwa kukumbukia machungu inamtosha kusoma neno lake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١﴾

“Hausibu msiba wowote isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na yeyote   anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoza moyo wake. Na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.” [ At-Taghaabun: 11] 

  

WabiLLaahi At-Tawfiyq       

 

 

 

 

Share