Ndizi Mbivu Za Kukaanga

Ndizi Mbivu Za Kukaanga

Vipimo

Ndizi mbivu zilizowiva sana - 4

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kataka ndizi kila moja kiasi ya vipande vitatu.
  2. Menya maganda, kisha kata kila vipande kwa urefu vitoke kiasi  vipande vitatu kutegemea na ndizi yenyewe. Ikiwa ni nyembamba, kata mara mbili tu.
  3. Weka mafuta kiasi kidogo tu katika kikaango (frying pan) kisha kaanga ndizi.
  4. Zinapowiva upande mmoja geuza upande wa pili kaanga kisha zitoe uweke katika sahani zikiwa tayari.

 

 

 

Share