Pizza Ya Samaki

 

 

 

 

Vipimo

 

Tuna steki wa kopo (oiled)                                        180 – 185 g 

 

Tomato ya kopo(paste)                                            3 Vijiko vya supu

 

Kitunguu maji                                                           1

 

Chumvi                                                                    1 kijiko cha chai

 

Unga wa ngano                                                        4 vikombe

 

Mafuta ya zaituni                                                      Nusu kikombe

 

Hamira                                                                    1 kijiko cha chai

 

Cheese ya Pizza                                                        100 g

 

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 

  1. Katika bakuli kubwa tia unga, hamira,mafuta na chumvi.Kisha mimina maji kidogo kidogo hadi mchanganyiko uwe donge la kunata kiasi tu. 

  2. Funika na uwache unga kwa muda wa nusu saa kisha ukande tena kiasi ukijipaka mafuta mikononi, ufinike kwa muda wa  masaa manne hadi sita.

  3. Ukishaumuka kufura itakuwa tayari kwa kuandalia vitu vya kuweka juu.

  4. Mimina tuna kwenye sahani huku ukichambua kuzidisha vijipande pande.

  5. Katakata kitunguu slesi nyembamba kando, tomato (paste) ndani ya kijibakuli tia maji vijiko 2 vya supu kisha koroga ili iwe kidogo nyepesi.

  6. Pake siagi au mafuta kiasi katika treya utakayochomea.

  7. Chukuwa unga ulioumuka ukande ufanye donge moja  na limwagie unga mkavu.

  8. Litandaze donge kwenye treya mpaka upate chapati kubwa kwa mikono bila kutumia kifimbo.

  9. Mwagia tomato (paste) kwenye pizza utandaze ,kisha  tuna halafu tupia vitunguu na utamalizia na  cheese.  

  10. Choma  kwenye oveni kwa moto wa 200°C  kwa muda wa dakika  25. Kisha unaweza kukata (shape) upendayo na

    itakuwa tayari kuliwa.

 

Kidokezo:

 

 Ukipenda  pilipili za kuwasha unaweza kuongezea na pia unaweza kutumia brokoli badala ya tuna.Ni vizuri kuliwa ikiwa moto moto. 

 

 

Share