Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)

Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)

   

 

Vipimo

Unga - 2 Magi (vikombe vya chai)

Sukari iliyosagwa - 2/3 Magi (kikombe cha chai)

Siagi   - 220 g

Unga wa mchele -  ½ Magi              

Yai -1

Vanilla  - 1 kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
  2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in)
  3. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu.
  4. Epua  acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.

Kidokezo:

Kwa unga huo huo unaweza kutengeneza vibiskuti vya duara duara.

 

 

 

 

Share