009-Unawezaje Kuupata Moyo Wa Mumeo Na Kumridhisha Mola Wako: Asiyemshukuru Mume Wake, Hamshukuru Mola Wake

 

ASIYEMSHUKURU MUME WAKE, HAMSHUKURU MOLA WAKE

 

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema,

“Mwenyezi Mungu Hamuangalii mwanamke ambaye hamshukuru mume wake na wakati huo huo hawezi kufanya lolote bila ya mumewe”[1]

 

Ewe mke mkarimu wa Kiislamu, kwa hakika mume wako anapigana na maisha magumu na kupambana ili kupata tonge la maisha na baada ya hapo anabeba mzigo wa familia, hivyo mdhanie vizuri daima, mshukuru yeye na Mola wako daima, wala usikikosoe kile akiletacho kwa ajili yako na ya familia, usikidharau na kukishusha thamani yake na kutokuridhika kuishi pamoja nae.

 

Tunamuona Mtume wa Mwenyezi Mungu Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) alipokwenda kumtembelea mwanae Ismaa’iyl (‘Alayhis Salaam) na hakumkuta baada ya kufika kwake na kumkuta mke wake, akamuuliza kuhusu hali zao na mke akajibu kuwa wapo katika dhiki, Ibraahiym akajua kuwa mke wa mwanawe hayuko radhi na maisha wanayoishi na mwanawe, hivyo akaamua kumuachia salamu mwanae kwa kumwambia mke wa mwanae, “Akija Ismaa’iyl mpe salamu zangu, na umwambie abadilishe kizingiti cha mlango wake.” Pindi alipokuja Ismaa’iyl, mke wake akamueleza yaliyojiri na kumpa salamu zake ya kuwa amekuja mzee akamuulizia hali yake, na akampa salamu zake na kumtaka Ismaa’iyl abadilishe kizingiti cha mlango, Ismaa’iyl akamwambia mke wake, “Yule ni baba yangu na wewe ni kizingiti cha mlango, nenda kwa jamaa zako”[2][1] Ameipokea Al-Haakim na akaisahihisha

[2] Tumeelezea mapokezi yake hapo nyuma

Share