015-Unawezaje Kuupata Moyo Wa Mumeo Na Kumridhisha Mola Wako: Wewe Ni Mchungaji Katika Nyumba Ya Mume Wako

 

WEWE NI MCHUNGAJI KATIKA NYUMBA YA MUME WAKO, NA UTAULIZWA KUHUSU UCHUNGAJI HUO

 

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema,

“Ee!! Jueni ya kwamba nyie nyote ni wachunga na kila mmoja ataulizwa alichokichunga, kiongozi wa watu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga, na mwanamme ni mchunga wa familia wake na ataulizwa kwa alichokichunga, mwanamke ni mchunga wa nyumba ya mume wake na watoto wake naye ataulizwa alichokichunga, na mtumwa ni mchunga wa mali ya bwana wake naye ataulizwa kuhusu uchungaji wake”[1]

 

Fahamu ewe dada wa Kiislamu kuwa nyumbani kwako kuna majukumu makubwa mno, kwa hivyo yahifadhi vizuri, muhifadhi vizuri mume wako na watoto wako. Hifadhi nzuri ya mali huwa ni katika mipango mizuri bila kufanya ubadhirifu. Ama kuhifadhi watoto maana yake ni kukesha kwa ajili yao ili wapate raha, na kuwalea malezi mema ya imani, ucha Mungu, uadilifu na kutekeleza ahadi.[1] Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslm

 

Share