Hijja Yake Imekubaliwa Ikiwa Amekwenda Bila Mahram?

 

Hijja Yake Imekubaliwa Ikiwa Amekwenda Bila Mahram?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Swali:

 

Assalaamu Alaykum,

 

Ndugu Zangu, Naomba Kukuliza Haba Ri Ya Mwanamke Kwenda Hajj Peke Yake.  Mimi Nimeenda Mwaka Jana.

 

Sikufuatana Na  Muhreem  Kwani Nimefiliwa Na Mume Wangu.,Wala Ndugu  Wala Mtoto.....Etc Yaani Nimetia Niya Tangu 1984  Pamoja Na Mume Wangu  Lakini  Sikuitika Labbaika  Wana Vyosema Watu. Na Mtoto Wangu Wa Kiume Anaeishi Nje  Tangu Kufa Mume Wangu   2000  Anani Himiza Kwenda Hija Na Mimi Siku Zote Namkatalia Kwa Kujua Kwamba Mwanamke Hawezi Kwenda Hija Pekeyake.   Nimejaribu Kuwauliza   Wasomi Wa  Dini  Yetu Na Nime Jibiwa  Kuwa   Mpaka Lini  Hata Niwapate Hao Ninaeweza.

 

Kufuatana Nao Na Umri Ni Huu Unakwisha Uwezo Nnao Kwa Fedha Na Siha. And So Nime Tawwakkal   Na Nime Fuzu. Sasa Suali Langu Ni Hivi   Hija Yangu Imekubaliwa?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukran kwa swali lako hilo na ni maarufu kwa kila mmoja kuwa nguzo ya Hijjah ina masharti yake ambayo yanafaa yatimizwe kabla ya kukubaliwa amali hiyo. Masharti ni kama yafuatayo:

 

  1. Muislamu.
  2. Aliyebaleghe.
  3. Mwenye akili timamu.
  4. Aliye huru (si mtumwa).
  5. Mwenye uwezo wa kwenda katika safari.
  6. Afuatane na mahram ikiwa ni mwanamke (hili ni sharti).

 

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma) amesema amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Asikae faragha mwanamme na mwanamke isipokuwa awe na mahram yake wala asisafiri mwanamke ila awe na mahram wake pia”. Akasimama mtu mmoja na kuuliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Mke wangu ametoka kwenda kuhiji nami nimejiandika kwenda jihadi kadhaa”. Alasema: “Nenda ukahiji pamoja na mke wako” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Baadhi ya Wanachuoni wameweka kuwa mwanamke kufuatana na mahram ni sharti na ndio kuweza kwake. Miongoni mwao ni Abu Haniyfah na wanafunzi wake, an-Nakha‘iy, al-Hasan, ath-Thawriy, Ahmad na Is-haaq.

 

Na mashuhuri kwa Imaam Shafi‘iy kuwa ameweka sharti ya kuwa mwanamke ni lazima aende Hijjah pamoja na mume au mahram au wanawake wengine waaminifu. Na kauli nyengine ni kuwa mwanamke mwaminifu anaweza kwenda peke yake. Na mwenye Subulus Salaam amesema kuwa kipote cha 'Imamu wamesema inafaa kwa mwanamke mkongwe kwenda safari hiyo bila ya mahram.

 

Na rai ya kamati ya wanachuoni iliyopo Saudia wamesema: Mwanamke ambaye hana mahram hana lazima kufanya Hajj kwa sababu kuwa na mahram ni mojawapo ya uwezo wa kwenda kutimiza nayo ni sharti ya ambayo Hajj huwa imewajibika kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

((وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً))

((Na kwa ajili ya Allah imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezaye njia ya kwendea.)) [Al-Imraan: 3:97]

 

Wenye kuruhusu mwanamke kwenda peke yake ni ile Hadiyth ya ‘Adiy ibn Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia kuwa ukiishi muda mrefu utamuona mwanamke kwenye hawdaj akisafiri kutoka Hirah mpaka kutufu Ka‘bah hamuogopi yeyote ila Allaah [Al-Bukhaariy].

 

Imaam Ibn Taymiyah amesema kuwa Hijjah ya mwanamke bila ya mahram inasihi.  Hao wanaonelea kuwa inawezekana mwanamke kusafiri na kundi kufanya Hajj, na wengine wamesema kuwa ikiwa mwanamke ni mwenye umri mkubwa pia anaweza kwenda na kundi la wenzake.

 

Kwa kulinganisha hoja zote mbili na dalili zao, tunashauri ni bora kuwa na mahram ili uweze kwenda kufanya Hajj, na kama huna mahram, basi hupaswi kufanya Hajj na utalipwa kwa nia yako kama ya yule aliyefanya Hajj inshaAllaah.

 

 

Mwanamke Kumfanyia Hijja Mtu Bila Ya  Mahram  

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share