Maharage Ya Sosi Ya Nyanya

Maharage Ya Sosi Ya Nyanya

Vipimo

Maharage - 1 Kopo 

Kitunguu - 1 

Nyanya - 1 Kubwa 

Pilipili mbichi-  1-2 

Nyanya ya kopo -  ½ Kijiko cha chai 

Pilipili ya unga - ¼ Kijiko 

Chumvi - Kiasi 

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai                                              

Kidonge cha supu -  ½ Kidonge 

Mafuta ya zaituni - 4 Vijiko vya supu 

Maji - Kiasi  

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Roweka maharage, kisha chemsha hadi yawive na kulainika; ikiwa unatumia maharage ya mkebe hakikisha unayaosha kwanza.
  2. Katika sufuria, tia mafuta na kaanga kitunguu na thomu mpaka ibadilike rangi na sio kuungua.
  3. Kisha tia nyanya (tungule) aina zote mbili, pilipili ya unga na pilipili mbichi, kidonge cha supu na maharage na ufunike na iache katika moto wa kiasi na usikoroge.
  4. Yakisha kaangika, utayaponda ponda, kisha tia maji ya kiasi na iache itokote kidogo.
  5. Halafu epua motoni na itakuwa tayari kwa kuliwa na mkate au chapati.
Share