Sevai Kee Kheer - Tambi Za Maziwa-2 (Pakistani)

Sevai Kee Kheer -  Tambi Za Maziwa-2  (Pakistani)

Vipimo          

Siagi - 2 vijiko vya supu

Tambi nyembamba sana za brown (Vermicelli) - 200 gm

Maziwa ya ng’ombe - 3 vikombe

Maziwa ya kuvukiza (evaporated milk) - 2  vikombe

Zabibu kavu -  ½ kikombe

Sukari - 3 vijiko

Lozi (zilizomenywa na kukatwa ndogondogo) - ½ kikombe

Hiliki -  1/3  cha chai 

Vanila au arki ya rose - 3 tone 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka siagi katika sufuria ishike moto.
  2. katakata tambi vipande vitatu na uweke katika ssfuria na ukaange kwa muda hadi kuwa rangi ya hudhurungi
  3. Tia maziwa na punguza moto uwe wa wastani acha ichemke
  4. Kisha weka sukari, zabibu kavu, lozi, hiliki, vanilla au rose
  5. Endelea kupika kwa muda wa dakika 5
  6. Ongeza maziwa glass  moja au mbili baridi na endelea kukoroga kwa muda kiasi
  7. Epua na weka pembeni ipoe kwa muda na ongeza maziwa baridi ili ichanganyike na isigandane. Koroga na ongeza maziwa ikibidi hadi iwe nyepesi kiasi
  8. Unaweza kula ikiwa moto au unaweza kuiweka katika friji ili iwe  baridi.   

 

 

Share