Kheer - Pudini Ya Mchele (Pakistani)

Kheer - Pudini Ya Mchele (Pakistani)

Vipimo  

Mchele wa basmati - ½ Kikombe 

Siagi - 1 Kijiko cha chai 

Maziwa mazito (full cream milk) - 4 Vikombe 

Iliki - ½ Kijiko cha chai 

Sukari -  ½ Kikombe au zaidi 

Zaafarani au vanilla - Kidogo 

Lozi na njugu (pistachios) zilizosagwa sio sana - 1 Kikombe 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Osha mchele na roweka kiasi ya nusu saa.
  2. Katika sufuria, tia siagi iache ipate moto, tia mchele na ukoroge.
  3. Kisha mimina maziwa na iwache ichemke pole pole kwa muda wa nusu saa hivi.
  4. Tia zaafarani (ukipenda), iliki na sukari.
  5. Iwache ichemke kwa muda wa dakika 10 zaidi.
  6. Halafu tia lozi na njugu, changanya vizuri kisha mimina kwenye vibakuli na iyache ipate baridi na tayari kuliwa.
Share