Mbaazi Za Nazi 2

Mbaazi Za Nazi -2

Vipimo 

Mbaazi za kopo -  2 

Kitunguu -  1 

Chumvi - kiasi  

Manjano - ½ kijiko cha chai  

Kidonge cha supu - kipande kidogo  

Mafuta -  1 kijiko cha chai  

Pilipili mbichi -  2 nzima  

Nazi  - 3 ½ vikombe   

Namna Ya Kutayarisha Na kupika  

1. Osha mbaazi kwenye chungio na ziache zitoke maji. 

2. Kaanga kitunguu kidogo tu kisha tia mbaazi na majano. 

3. Tia kidonge cha supu na chumvi pilipili mbichi na nazi

    vikombe vitatu, utabakisha nusu kikombe. 

4. Ikisha kauka kidogo changanya nazi ya unga kama

    vijiko 4 vya supu kwenye nazi uliobakisha, mimina kwenye mbaazi. 

5. Iache motoni kidogo hadi iwe nzito na itakuwa tayari kuliwa kwa maandazi.

 

 

Share