Keki Ya Cherry

Keki Ya Cherry

Vipimo  

Siagi - 400g 

Unga - 4 Vikombe 

Sukari - 200g 

Mayai - 10 

Baking powder - 2 Vijiko vya chai 

Cherry - Unazotaka 

Jam ya cherry -  Kiasi 

Vanilla - ½ Kijiko cha chai 

Mchapo wa malai (whip cream) - Kiasi 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Washa oveni moto wa 350°c
  2. Saga siagi na sukari kwa mashine mpaka mchanganyiko ulainike vizuri.
  3. Ongeza yai moja baada ya moja huku unaendelea kusaga hadi yamalizike.
  4. Tia unga uliochanganwa na baking powder.
  5. Tia vanilla endelea kuchanganya.
  6. Mimina mchanganyiko kwenye vyombo viwili tofauti vilivokuwa saizi moja.
  7. Vumbika (bake) kwenye oveni kwa muda wa dakika 20 – 25.
  8. Kisha iache ipoe kidogo, halafu weka keki zote mbili kwenye treya kubwa halafu mojawapo itoe sehemu ya juu kwa kisu (yaani yale magamba ya keki), halafu itandaze jamu keki nzima kisha weka cherry.
  9. Keki iliyobakia itowe sehemu ya chini kwa kisu (yaani yale magamba ya keki) halafu iweke juu ya ile keki ya uliopaka jam, hakikisha imekaa sawa, kisha paka mchapo wa malai (whip cream) juu yake na weka cherry na itakuwa tayari kuliwa.

Share