Kuku Mzima Wa Kuoka (Baked) Na Sosi Ya Ukwaju Na Vitunguu Kijani

Kuku Mzima Wa Kuoka (Baked) Na Sosi Ya Ukwaju Na Vitunguu Kijani

Vipimo 

Kuku - 1 mzima

Kitunguu saumu/thomu na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu

Chumvi - Kiasi

Bizari mchanganyiko - 2  vijiko vya supu

Pilipili mbichi kijani na nyekundu  -  2-3

Ukwaju  mzito uliokamuliwa - ½ kikombe

Vitunguu vya kijani (spring onions)  - 2 mche (stalk)

Kotmiri - 1 mche (stalk)

Mafuta - 1 Vijiko vya supu 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Safisha kuku kisha mwache achuje maji vizuri.
  2. Katakata vitunguu, pilipili, kotmiri, weka kando.
  3. Changaya masala yote kwenye bakuli pamoja na mafuta.
  4. Mpakaze  kuku wote masala ya ukwaju nje na ndani akolee viungo. Kisha roweka kwa muda wa masaa yasipungue mawili takriban. 
  5. Muweke katika treya, na bakisha sosi ulomrowekea kidogo kando.
  6. Mtie katika oveni na muoke (bake) katika moto wa  350º-400º kwa muda wa takriban dakika 45.  
  7. Akishaiva ongezea kumpakaza tena nje na ndani sosi ilobakia na nyingine mwagia juu yake. Mwagia vitunguu, pilipili kisha mchome moto wa juu (grill)  kwa muda wa dakika 5-8 huku unamgeuza mpaka abadike rangi. Ikiwa katika jiko la makaa huku ukimgeuza na ukimpaka mafuta kidogo kidogo na mchanganyiko wa urojo wa ukwaju kwa brashi.  

Kidokezo : Tolea na saladi, mkate na sosi ya hummus. Bonyeza kiungo kifuatacho: 

Hummus (Shaam)

 

Share