Bonus Accounts Ni Halaal Au Ribaa?

SWALI:

  

Asalam alaykum, je zile bonus accounts kama za NMB zaruhuiwa? Wabillaho tawfiiq!

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu bonus (nyongeza) unazopata kutoka kwa NMB. Ndugu yetu umeuliza swali lako kwa ujumla sana kwani hukutufahamisha hizi bonus mtu anapewa vipi.

 

Hata hivyo, shughuli za benki za kawaida zote zinafanya kazi zake kwa kutegemea Riba ambayo ni haramu Kiislamu. Kwa ajili hiyo huenda ikawa hii bonus ni jina jengine la Riba au kwa uchache kuna shaka ndani. Na hali ikiwa hivyo ni vyema kuacha lenye shaka kwa kufuata lisilo na shaka. Kwa hivyo, njia bora ni uichukue usiache makafiri kunufaika nayo lakini usiitumie kwa faida yako bali usaidie katika mambo yasiyo ya dini kama kujenga barabara, mifereji  n.k. bila ya kutarajia thawabu.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share