Vipi Wakimbizi Wajisafishe Na Uongo Wanaosema Serikalini?

SWALI:

 

ASALAMU ALYKUM

WENGI KATIKA SISI WAISLAMU TUMEHAMA MIJI NA NCHI ZETU NA KWENDA ULAYA, MAREKANI AU CANADA "KUTAFUTA MAISHA BORA"

 

HUKO ULAYA, MAREKANI AU CANADA, SERIKALI ZAO ZIJIMEWEKA SHERIA NA MISINGI YA NAMNA YA KUWAPOKEA WAGENI NA KUWAPA URAIA. WENGI WETU WAISLAMU TUMETUMIA MBINU ZA URONGO NA UJANJA, MFANO KUSEMA KWENU WAKANDAMIZWA KIDINI, AU KIKATIBA AU KISIASA. WENGINE WAMESEMA WAO NI WASOMALI, WABARAWA AU BAJUNI KUTOKA SOMALIA. UKISHA PITA MITIHANI (INTERVIEW) BASI WEWE UTAPATIWA CHETI CHA KUISHI NA PIA KUPOKEA PESA ZA MATUMIZI.

 

SWALI LANGU, JE, PESA HIZO NI HALALI? PILI URONGO HUO WATAFISIRIKA VIPI KIDINI? KAMA YOTE NI MAKOSA KIDINI YETU TUKUFU, JE NDUGU ZETU WATAJISAFISHA NA MAPESA HAYO YA HARAMU NA URONGO WA MIAKA MINGI?

 

WABILLAHI TOWFIQ 

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu wakimbizi kujisafisha na uongo wanaosema serikalini.

Tufahamu kuwa mwanzo ukweli ni sifa muhimu sana ambayo Muislamu anafaa kuwa nayo katika maisha yake na katika hali zote. Ndio Allaah Aliyetukuka Akatuambia: “Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na kuweni pamoja na wakweli” (at-Tawbah 9: 119).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuarifu kuwa Muumini hawezi kuwa muongo kabisa.

 

Tufahamu kuwa pesa zinazopatikana kwa uongo si halali kwa mwenye kupatiwa kabisa. Wale waliopata pesa hizo inabidi wajisafishe na kwa hiyo waombe maghfira kutoka kwa Allaah Aliyetukuka. Katika kukubaliwa toba ni lazima mtu afanye yafuatayo:

 

1.     Kujiondoa katika maasiya hayo. Kwa hiyo kuanzia sasa asiwe ni mwenye kuchukua tena pesa hizo.

 

 

2.     Ajute sana katika kufanya kosa hilo.

 

 

3.     Aazimie kutolirudia tena kosa hilo.

 

 

4.     Na kwa kuwa amechukua haki ya mwanaadamu ni lazima arudishe hicho alichochukua, katika swali hili ni pesa. Kwa kuwa huenda kuzirudisha moja kwa moja inaweza kumletea shida kutoka kwa serikali ni lazima atafute ya kuweza kuzirudisha kwa njia moja au nyingine.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Nasaha Kwa Wakimbizi Wanaoishi Kusema Hawajaoana Ili Wapate Ruzuku Ya Serikali

 

Wamesema Uongo Serikalini Kuwa Hawakuoana Wapate Pesa, Huku Wameoana Kikweli Je, Watoto Wao Ni Halali

 

Pesa Anazopata Kwa Kuongopa Serikalini Zinafaa Kutumika Kwa Matumizi yake na kufanyia Mambo Ya Kheri?

 

 

 

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atuepushe na uongo ili tusiingie katika matatizo hayo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share