02-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Abdullah Ibn Saba'i

 

Hakika inavyo julikana kwetu sisi mashia kuwa ABDULLAH IBN SABAI ni mtu wa kubuni hatambuliki kuwepo kwake, wamemtengeneza AHLUS SUNNAH, kwa ajili  ya kuutia hila ushia na imani yake,wakamnasibishia (Bin Sabai ) kuanzilishi ushia ili wawazuie watu kuingia ushia, nakutofuata madhehebu ya AHLUL-BAYT. Na nilimuuliza Bwana Mohammad Ali kaashiful-ghatwaa kuhusu IBN SABAI akasema,  kuwepo kwa mtu aitwae Ibni Sabai ni kitendawili kisichokuwa na ukweli wowote  wamekitunga Ummawiya na Abasiyya kutokana na husda zao dhidi ya Ahlul-Bayt walio takasika,basi inatakiwa kwa mwenye akili asijishughulishe na habari za  mtu huyu.

Lakini mimi nimeona katika  kitabu  chake maarufu kinachoitwa (ASILI YA USHIA NA MISINGI YAKE)ukurasa 40-41,maneno yanayoonyesha  kuwepo kwa mtu huyu, na uhakika wake pale aliposema  “Ama Abdullahi bin Sabai ambae wanamuhusisha na ushia au wanauhusisha ushia kwake, basi vitabu hivi vyote vya ushia  vinatangaza kumlaani na kumkataa......” na hakuna shaka yeyote  kwamba huu   ni ushahidi wa kuepo kwake (Bin sabai) Na nilipomrudia kutaka ufafanuzi wa maneno haya, alisema: sisi tumesema hivi kwa njia ya Taqiyya tu (kudhihirisha kinyume cha ulicho nacho) kuhusu kitabu ulicho kitaja kimekusudiwa  AHHLU SUNNA, (na wala si mashia) na kwa ajili hii nimefuatilia usemi wangu ulio tajwa kwa kusema baadala yake:(kuwa sio mbali mawazo yanayosema kuwa Abdillahi Bin sabai,na wale wanaofanana nae vyote hivyo ni vigano visivyo na uhakika wowote wameviweka wasimulizi na wakuu wa mazungumzo ya paukwa pakawa).

Na alitunga bwana Murtadha Al Asakariy kitabu chake (ABDALLAH BIN SABAI NA VITENDAWILI VINGINE) ndani yake amekanusha  kuwepo kwa ibn saba, pia SHEIKH MUHAMMAD JAWAAD MUGHNIYA, kakanusha kuwepo BIN SABAI  katika  utangulizi wake wa kitabu cha  sayyid Murtadwa kilicho tajwa.

Na Abdallah bin sabai ndie sababu mojawapo ambayo inawafanya hasa watu washia kuwa na chuki dhidi ya AHLUS SUNNAH  Na bila shaka  wale walio mzungumzia Ibn Sabai miongoni mwa AHLUS SUNNAH hawahesabiki , lakini mashia hawazizingatii kauli za wanachuoni wa kisunna  kutokana na tofauti zilizopo kati yao, isipokuwa tunapo soma vitabu vyetu vinavyotegemewa (katika ushia) tunaona kuwa ibn sabai  ni shaksiya ya uhakika wajapoipinga wanazuoni  wetu  au baadhi yao na huu ndio ubainifu  wa hilo:

1.    Imepokewa kutoka kwa Abii Jafar (a.s) kwamba Abdalllah bin saba alikuwa akijitangazia utume, na akidai kuwa kiongozi wa waislamu (Ali) ndie Mungu ametukuka  Mungu kwa hilo, madai hayo yakamfikia Ali (a.s) basi akamwita na akamuuliza,akakiri na kusema :ndio wewe ndiwe hasa,kwani nimepata ufunuo katika moyo wangu kuwa wewe ni Mungu, nami ndie Nabii, hapo  akasema Ali (a.s)ole wako shetani amekuhadaa,rudi kutokana na haya (yaani acha madai haya)atakukosa mama yako, na utubu,nae akakataa, akamfunga na akamtaka atubu kwa muda wa siku tatu, nae hakua atayari kufanya hivyo akamuunguza kwa moto na akasema  :( hakika sheitani amemghuri,alikua akimuendea na kumuekea moyoni mwake mambo hayo).

Na anasimulia Abii Abdallah kwakusema:(Mwenyezi Mungu amlaani Abdallah bin sabai,kwani yeye alimtangazia Uungu kiongozi wa waislamu Ali (a.s), na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu  Amiril  muuminin Ali (a.s) nimja wa Allah, mtiifu,ole wake yule anae tusingizia uongo,kwani baadhi ya watu wanatusemea yale ambayo hatuyasemi hata katika nafsi zetu tuna jitakasa kwa Mwenyezi Mungu na hao,tuanajitakasa na Mwenyezi Mungu na hao) (MA’RIFATU AKHBARU ARIJAL) ukurasa 70-71. na pia kuna mapokezi mengine.

 

2.    Na amesema Almamuqani:( Abdallah bin sabai ndiye ambae amerejea kwenye ukafiri na akatangaza kuvuka mipaka) na akasema:( amelaaniwa ,amevuka mipaka, Amirii –muuminin alimteketeza kwa moto,  pia alikuwa akidai kuwa Ali ni Mungu na yeye ni Nabii)  TANQIYHUL- MAQAL FII  ILMIL RIJAL) JUZUU 2 / 183-184.

 

3.    Na amesema ANNAWBAKHTY( wafuasi wa bin sabai ndio walioanza kuzungumza kuhusu uimamu wa Ali na kusema kuwa uimamu wa Ali ni faradhi kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Bin sabai ni katika watu walio dhihirisha tuhuma kwa Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan na maswhaba wengine  na kujitenga nao na akasema kuwa Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuamrisha hivyo) basi Ali (a.s) alimkamata na kumuhoji kuhusu maneno yake haya, akakiri,Ali akaamrisha auwawe, watu wakampigia kelele Ali na kumuambia  ‘Ewe kiongozi wa waumuni unataka kumuua mtu anaewataka watu wakupendeni AHLUL BAYT, na kutaka uongozi wako na kujitenga na maadui zako, basi akamuhamisha katika miji mingine, wanasimulia jamaa miongoni mwa wanazuoni kuwa Abdallah bin sabai alikuwa myahudi akasilimu,na akadai kumpenda Ali (a.s) na alikuwa akisema  alipokua katika uyahudi wake kuhusu Yushiu bin nuun, baada ya Musa (a.s) maneno haya  na  akaja kutamka baada ya kusilimu maneno hayahaya kuhusu  Ali bin  Abii Twalib . Nae ndie mtu wa mwanzo aliedhihirisha usemi wa kuwa uongozi wa Ali (katika uislamu) ni lazima,  na kudhihirisha uadui kwa maadui zake Ali,na kwa sababu hii wanasema watu wenye kuupinga ushia asili yake ni uyahudi. kuanzia hapa anasema mwenye kwenda kinyume na shia asili yake ni uyahudi (FIRAQU ASHIAH)uk 32-44.

 

4.    Na amesema Sa’ad bin Abdillah Al-ash’ariy Al qumiy katika mwanzo maneno yake kuhusu wafuasi wa bin sabai:( Assabaiyah ni wafuasi wa Abdillah bin sabai, nae anaitwa Abdallah bin Wahab Arraasibiyyi Al-hamdany ,na alisaidiwa katika mpango wake na Abdallah bin kharsy na bin As-wad,na watu wawili hawa ni katika wafuasi wake wakuu. Na alikuwa wa kwanza kuonesha wazi kuwatusi Abu bakar,’Umar na ‘Uthmaan na masahaba wengine na akatangaza uadui nao) (ALMAQAALAT WALFIRAQ)uk 20.

 

5.    Amesema swaduuq: Amesema Amiril-muuminina (a.s) “Akimaliza mmoja wenu kuswali naanyanyuwe mikono yake juu na ajitahidi kumuomba mungu,basi akasema bin sabai:ewe amiril-muuminina hivi mwenyezi mungu hayupo kila mahali?akasema(Ali)kwa nini isiwe hivyo? Akasema (bin sabai)kwa nini basi mtu anyanyue mikono yake juu? Akasema (Ali)

kwani wewe husomi maneno ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) yasemayo: " وفي السماء رزقكم وما توعدون"(na katika mbingu kuna rizqi yenu na mliyo ahidiwa) basi wapi mtu ataitafuta rizqi zaidi ya mahali pake? Na mahali pa riziqi palipo ahidiwa na Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ni mbinguni. (MANLLAA YAHDHURUHUL-FAQIIH, 1/229).

 

6.    Amesema bin Abil-hadyd kuwa Abdallah bin sabai  alimuendea  Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu)  huku akiwa anhutubia watu kisha akmwambia( wewe wewe naakawa anarudia rudia kusema hivyo),Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia (una nini wewe?  mimi nani?)akasema :wewe ni  Mungu. Basi akaamrisha akamatwe yeye na watu walio pamoja nae katika mawazo yake.(SHARHU NAHJUL BALAGHA)  juzuu ya 5 / uk 5.

 

7.    Na Assayid  Nematullahi Aljazaairiy, amesema:( Abdallah bin sabai aliesema kumwambia Ali (a.s) hakika wewe ndie Mungu wa kweli, Ali(a.s) akamuamisha kumpeleka Madaainu, na  inasemekana kwamba alikuwa myahudi akasilimu,  pia alipokua katika uyahudi alikuwa  akisema khusu  Yushi’u bin nun, na musa maneno kama haya aliyo yasema kwa Ali(a.s)  (AL-ANUWARU ANNU’U MAANIYYA)juzuu ya 2/ uk 234, basi hizi ni dalili saba (zinazothibitisha kuwepo kwa bin sabai katika ushia) zilizopatikana  kutoka kwenye vitabu vinavyotegemewa vya kishia  baadhi yake vinahusu Elmul-Rijaal(elemu ya kuwatambuwa watu)  na baadhi yake katika fiqhi na madhebu mbalimbali, baja na hivyo tumeacha kunukuu kutoka kwenye vitabu vingine ili tusirefushe, vitabu vyote hivyo vinathibitisha kuwepo kwa mtu aitwae Abdallah bin Sabai.basi haiwezekani kwetu sisi baada ya hoja hizi kukanusha kuwepo kwa bin sabai kwa ushahidi kwamba Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alitoa adhabu kwa bin sabai kwa kumuita mungu  kwa maana hiyo inathibitika kwamba Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikutana na bin sabai, basi hiwezekani kukanusha kuwepo bin sabai baada ya hoja hizi.

 

 

 

 

 

Share