04-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Mut'ah Na Yanayohusiana Nayo

 

Nilikuwa nataka kuweka anuani ya sehemu hii kua ni {MWANAMKE KATIKA USHIA} lakini nikaibadilisha  anuani hiyo kwa sababu nimeona mapokezi yote yanayopatikana katika vitabu vyetu yananasibishwa (yanaegemezwa) kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kwa Amiril muiminina na kwa Abii abdillah (‘Alayhis Salaam) na wengineo miungoni  mwawanazuoni.

Na mimi sikutaka wana zuoni hao wapatwe na lawama za aina yeyote ile kwani katika riwaya hizo  kuna maneno machafu ambayo mtu yeyote hawezi kuyaridhia katika nafsi yake, vipi mtu atayaridhia maneno hayo kwa mtume  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au atawezaje kuyaridhia kwa Ali wa mtume au kwa maimamu watukufu  (amani ya mungu iwashukie)

 

Hakika mut’a imetumika vibaya sana  na mwanamke amedhalilishwa  (kwa sababu ya dhana ya uhalali wa mut’a) udhalilishaji mbaya sana,watu wengi wakawa  wanakidhi matamanio yao ya kimwili chini ya pazia ya mut’a,na kutumia jina la dini,wakilitumia neno lake Mwenyezi Mungu lisemalo:

   {....فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة....}

{Mtakapostarehe nao baada ya kufunga nao ndoa basi wapeni mahari yao kwani ni lazima kuwapa} Annisaai 24.

 

Zimepokewa riwaya nyingi kutoka kwa mashia zinahimiza  mut’a  mpaka wakafikia  kuweka thawabu kwa mwenye kufanya mut’a na madhambi kwa mwenye kuacha mut’a,na inazingatiwa kila asiefanya si muislamu (kwa mtazamo wamashia)

 

Soma pamoja na mimi ushahidi huu:

 1. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): {Atakae starehe (kufanya mut’a) na mwanamke muumin atakua sawa na aliyezuru Al-kaaba mara sabini} inawezekanaje mtu alie strehe na mwnamke awe ni kama alie zuru Al-kaaba mara sabini?

 

 1. Amepokea Asuduq kutoka kwa Asadiq amesema {Hakika mut’a ni dini yangu na dini ya baba zangu atakaeifanya  (mut’a)atakuwa  amefanya hivyo kwa kufuata dini yetu na atakae pinga (mut’a)atakuwa ameipinga dini yetu na atakuwa na imani tofauti na imani yetu} MANLA YAHDHURUHU AL-FAQIYH 3/366, na huku ni kumkufurisha yule asiyekubali mut’a.

 

 1. Aliulizwa Abu Abdillah (‘Alayhis Salaam) je mwenye kufanya mut’a anapata thawabu?akasema: {ikiwa anafanya hivyo kwa kutaka kupata radhi za Mwenyezi Mungu basi kila neno atakalomsemesha  (huyo mwanamke aliyefanya nae mut’a) Mwenyezi Mungu atamuandikia jema moja, atamkaribia, mwenyezi mungu atamsamehe dhambi moja, na atakapooga husamehewa madhambi kiasi cha maji yaliyopita katika nywele zake} MANLA YAHDHURUHUL AL-FAQIYH 3/366.

 

 1. Na amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): {atakaejistarehesha (kufanya mut’a) mara moja atsalimika  na hasira za Mwenyezi Mungu, na atakae fanya (mut’a) mara mbili atafufuliwa pamoja na watu wema, na atakae fanya (mut’a) mara tatu atakua pamoja  nami peponi}MANLA YAHDHURUHUL AL-FAQIYH 3/366.

 

Ninasema: kwa ajili ya   kupata thawabu hizi  (za mut’a)  walimu wote wa hapa chuoni na viongozi pamoja na wanawake wazuri waliopo hapa chuoni wote wanafaya mut’a kwa wingi sana,na nakusudia   kutaja miongoni mwao bwana ALSADRU- NA AL-BARO JARDY- NA ASHIRAZY- NA ALQAZ’WAYN, NA ALTABATABAI, NA ASSAYID AL MADANIY, bila kumsahau kijana anaenyanyukia, ABDUL HARITH AL-YASIRIYI, na wengineo, hakika hao  (waliotajwa) wanafanya mut’a  kwa wingi  na kila siku  kwa hamu yakupata thawabu hizo (zilizo tajwa) na kutaka kua pamoja  na mtume peponi .

 

Na amepokea bwana FAT-HULLAHI ALKASHAANIY katika kitabu TAFSIR MINHAJI ALSADIQIYNA kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “atakae fanya mut’a mara moja atapata daraja ya Husain (‘Alayhis Salaam),na atakae fanya  mara mbili atapata daraja ya Hasan (‘Alayhis Salaam),na takae fanya mara tatu atapata daraja  ya Alli Bin Abii Talib (‘Alayhis Salaam),na atakae fanya mara nne atapata daraja yangu”

 

Tuchukulie mtu mmoja mchafu ataamua kufanya mut’a mara mmoja hivi kweli ataweza kupata kama ya Husain?au akafanya mara  mara mbili au tatu au nne ataweza kuwa na daraja  (cheo) kama Hassan au Ali au  Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)?je cheo cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na vyeo vya maimamu wetu ni duni kiasi hiki?

 

Hata kama mtu anaefanya mut’a atakuwa amefikia ngazi ya ya juu katika imani hivi kweli ana weza kufikia cheo cha Husain au Hasan au Ali au Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)?!

 

Hakika daraja ya Husein ni ya juu sana hawezi kuifikia mtu hata akiwa imani kiasi gani,pia mtu hawezi kufikia daraja ya Hassan auAli auMtume hata kama imani yake ingekuwa juu vipi!

 

Wameiruhusu mut’a mpaka kwa wanawake wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kama ilivyo pokewa na  ATWUUSIYY katika kitbu (ATAHDHYB 2/193).

 

Basi ninasema kuwa jamaa zake mtume ni watukufu hawafanani kufanyiwa kitendo kama hicho  (mut’a) kwa sababu wao ni kizazi cha mtume  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na watu wa nyumbani kwake wanawezaje kufanyiwa kitendo kama hivho, na nitawatajia sababu ya hilo inshaa Allah.

 

Amebainisha kulainiyi kuwa mut’a inafaa japo kwa tendo moja la ndoa , kati ya mwanaume na mwanamke, na suala hili limeelezewa katika kitabu  FURUL-AL-KAFI 10/460.

 

Na si lazima mtu utakae fanya nae mut’a awe mkubwa bali inawezekana kufanya mut’a na mtoto wa miaka kumi, na kwa kuthibitisha hili, amepokea Al-Kulainiy katika kitabu AL-FURUI juzuu ya 5 uk. 463 pia amepokea Attaausiy katika kitabu ATTAHDIYB 7/255 kua aliulizwa Abii Abdillah (‘Alayhis Salaam):  {msichana mdogo je inafaa kufanya nae mut’a? Akasema ndio,isipokua mtoto mdogo anae weza kudanganywa, akaulizwa ni umri gani ambao hawezi kudanganyika, akasema miaka kumi}.

 

Na hoja zote hizi zitapatiwa majibu Mwenyezi Mungu akipenda, lakini ninasema: yote yaliyo nasibishwa kwa Abii Abdillah yanaonyesha kuruhusu mut’a kwa msichana mwenye miaka kumi, lakini baadhi yao wamefikia kuruhusu mut’a kwa msichana aliye chini ya miaka hiyo.

 

Alipokuwa imama AL KHOMEINI akiishi  Iraq tulikua tunaenda kwake kupata Elimu mpaka ukawa uhusiano wetu na yeye ni mkubwa sana ,na ilitokea siku moja kukubali mwito wa kuutembelea  mji TAL-AFAR, (tal-afar ni mji ulio magharibi mwa mji wa AL-MUUSWAL) kiasi cha mwendo wa saa moja na nusu kwa gari, akaniomba nisafiri nae,nikasafiri nae,wakatupokea na wakatukirimu takrima iliyo kubwa kwa muda tuliokuwa kwenye familiya moja ya kishia yenye kukaa huko na  walikubaliana kueneza ushia sehemu hiyo,wanaendelea kuzihifadhi picha za ukumbusho tulizo piga nao nyumbani kwao.

 

Na ulipomalizika muda wa safari tulirudi,na tulipokua tuna rudi tukipitia Baghdadi alitaka imamu tupumzike kutoka na na uchovu wa safari, akaamrisha tuelekee katika mji wa Al-atafiya anapokaa mtu mmoja mwenye asili ya kiirani aitwae  Sayid Swahib ambae alikuwa akifahamiana sana na imama Khomeini.

 

Akafurahi sana Sayid Swahib kwa kuja kwetu,na tulifika kwake wakati wa Adhuhuri,akatuandalia chakula cha fakhari,akawasiliana na jama zake wakahudhuria, na wakajaa katika nyumba ile kwa kutukirimu sisi,na akatutaka Sayid Swahib usiku ule tulale kwake, na akakubali imamu khomeniy hilo, na ilipofika wakati wa isha tuliletewa chakula cha usiku,wakawa walio hudhuria wanaubusu mkono wa imamu, na kumuuliza mas-ala na akiwajibu mas-ala yao, na ulipokaribia wakati wa kulala na waliohudhuria wameshaondoka,isipokua wenye nyumba, imamu  KHOMENEI alimuona binti wa umri wa miaka minne au mitano,mzuri sana imamu akamuomba  baba yake mtoto  (sayd swahib) amlete ili afanye nae mut’a  baba yake mtoto akakubali kwa furaha kubwa, basi akalala imamu khomeni na yule msichana akiwa mapajani kwake, huku tukisikia kilio chake na kelele zake!!

 

Usiku  ule ulipita,ilipofika wakati waasubuhi,tulikaa na kunywa chai, akaniangalia imamu khomeniy na akakuta alama ya  kulipinga lile jambo waziwazi katika uso wangu,kwasababu vipi atafanya mut’a  na mtoto mdogo huyu wakati  katika nyumba ile kuna wasichana wakubwa wazuri anaoweza kufanya nao mut’a , kwa nini asifanye nao badala yake afanye na mtoto mdogo ?

 

Akaniambia: Sayid Husein umesema nini kuhusu kufanya mut’a na mtoto mdogo?nikamwabia : bwana wangu kusema ni kwako, na kitendo chako ndio sahihi , kwa sababu wewe ni imamu mwenye  kujitahidi,haiwezekani kwa mtu mfano wangu mimi  kuona au kusema isipokua ulivyoona wewe au ulivyosema, (nilisema hivyo kwa sababu wakati huo nisingeweza kupinga chochote)

 

Akasema: “Sikia Sayid Husein, hakika kufanya mut’a na mtoto mdogo inafaa lakini kwa kucheza nae na kum’busu na kumpitishia dhakari katika mapaja yake, kwa sababu tendo la ndoa haliwezi.

 

 Na alikua Imamu Khomeini akiona inafaa kufanya mut’a mtoto hata ane nyonya, akisema: {si vibaya kustarehe na mtoto anaenyonya kwa kumkumbatia na kuichezesha dhakari kati ya mapaja yake na kum’busu} tazama kitabu chake ATAHRIRU ALWASILA 2/24/ MLANGO, NAMBA 12.

 

Nilikaa katika ofisi ya imamu ALKHUUIY wakaingia vijana wawili yaonekana kuwa wametufautiana katika mas-ala Fulani waka afikiana kumuuliza imamu AL KHUNIY ili awafahamishe jawabu, akauliza mmoja wao, unasemaje imamu kuhusu mut’a? je ni halali au ni haramu? Akamuangalia  imamu AL KHUIY yule kijana huku akiwa amehisi  jambo katika swali lake,kisha akamwambia wapi unaishi?akasema yule kijana naishi Al mauswil,lakini sasa hivi niko hapa  Annajaaf inapata miezi miwili,imamu akamuuliza yule kijana : je wewe ni Ahlus Sunnah? Akasema kijana ndiyo, imamu akasema: mut’a kwetu sisi (mashia) ni halali lakini kwenu (Ahlus Sunnah) ni haramu,yule kijana akasema mimi nipo hapa yapata miezi miwili nikiwa mgeni katika mji huu,basi utaniozesha binti yako ili ni starehe nae mpaka nitapo rudi kwetu? imamu akanyamaza kidogo kisha akamwambia: mimi ni mtukufu na hili jambo ni haramu kwa watukufu,na ni halali kwa mashia wa kawaida

 

Kijana akamwaangalia Asayid AL KHUUIY huku  akitabasamu na  mtazamo wake unaonyesha kuwa kijana kafahamu kwamba imamu Al Khuuiy ametumia taqiya kisha wakasimama na kuondoka, nikamtaka rukhsa  imamu Al Khuuiy ya kutoka, nikakutana na wale vijana wawili,nikaelewa kuwa mwenye kuuliza ni Ahlu sunna na mwenzake ni shia wametofautiana juu ya mut’a je ni halali au  haramu? Wakaafikiana  juu ya kuuliza marejeo ya dini ya Al imamu Al khuuiy,nilipo wazungumzisha vijana wawili hao, yule wa kishia alipandisha hasira na kusema: Enyi watu waovu,mnaruhusu kustarehe na wasichana wetu, na mnatueleza kua ni halali na inawakurubisha,kwa Mwenyezi Mungu na  mnatuharamisha kustarehe na mabinti zenu? yule kijana akaondoka na huku  akitukana na kushutumu na akiapa kuingia katika madhehebu ya Ahlus Sunnah, nikawa namtuliza yule kijana na kumuapia kwa mungu kuwa mut’a ni haramu na nikampa ushahidi wa hilo.

 

Hakika  mut’a ilikua inafaa zama za ujinga, uislamu ulipo kuja  uliibakisha mut’a  kwa muda,kisha ikaharamishwa katika vita vya Khaibara, lakini  lililozoeleka kwa mashia na wasomi wao ni kwamba ‘Umar bin  Khatwaab ndie aliye iharamisha, na haya ndiyo yaliyoelezwa na baadhi ya wanazuoni wetu. 

Na ukweli ni kwamba mut’a iliharimishwa katika vita vya khaybar.

 

Amesema Amirul Muuminin (‘Alayhi salaam): {aliharamisha Mtume  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) siku ya khaybar  kula nyama ya punda wakufugwa na ndoa ya mut’a} tazama  (ATTAHDHB 2/186) (AL-ISTIBAR 3/142), (WASAILU AL SHIA 14/441).

 

Na akaulizwa Abuu Abdillah (‘Alayhis salaam): {Je walikuwa waislamu katika zama za mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakiona bila ya kutangaza? Akasema: hapana} (tazama ATTAHDHIYB 2/189).

 

Amesema At Tuusiy akifafanua maneno hayo; hakika Abu Abdillahi hakukusudia kwa maneno yake hayo ndoa ya kudumu isipokuwa alikusudia mut’a ndio maana ameyaleta maelezo haya katika mlango unaohusu mut’a .

 

Hakuna shaka kwamba hoja mbili hizi ni zenye kuifuta mut’a na kuibatilisha.

 

Amiril-muuminin  (‘Alayhis Salaam) ameelezea kuharamishwa mut’a  kutoka kwa mtume  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)  na hii ina maana  kuwa Amirul muuminin  (‘Alayhis Salaam) amesema kwamba  mut’a iliharamishwa tokea siku ya khaibara na bila  shaka viongozi wengine baada yake walijua hukumu  ya mut’a baada ya kuja kwao kuwa  imeharamishwa .  Na hapa tuko mbele ya habari aina mbili : zilizo pokewa zinazoeleza waziwazi kuhusu uharamu wa mut’a ,Na zile zinazo nasibishwa kwa maimamu zinazo himiza kufanya mut’a,  Na hili ni tatizo muislamu anachanganyikiwa afanye mut’a au asifanye?

 

Usawa ni kuacha mut’a  kwasababu ni haramu kama zilivyothibiti habari zake kutoka kwa   Amirul muuminin (‘Alayhis Salaam) ama maelezo yaliyo nasibishwa  kwa maimamu bila shaka si sahihi, bali ni habari za uzushi wamesingiziwa maimamu, (‘Alayhis Salaam) kwani hawawezi kwenda kinyume na jambo  alilo liharamisha mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam),na Amiril-muminina akawa na msimamo huohuo baada ya mtume  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ukizingatia wao ndio walio chukua elemu kutoka kwa mababu na mababu kwa sababu wao ni familia moja,

 

 

Alipoulizwa Abuu Abdillah (‘Alayhis Salaam): (Je walikuwa waislamu katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakioa bila ya kutangaza? Akasema:hapana, haikua hivyo)kama asingekua anajua kuwa mut’a ni haramu asingejibu kwa kusema hapana, hasa ukizingatia swali liliulizwa kuhusu mut’a  na kwamba Abu Jaafar alieipokea habari hii ameika katika mlango wa mut’a kama tulivuo sema.

 

Na haikuwa inawezekana  kwa Abii Abdillah (‘Alayhis Salaam) wala maimamu walikuwa kabla yake na baada yake  kwenda kinyume na amri ya mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au kuuhalalisha jambo aliloharamisha  au kuzua jambo  lisilo julikana  katika zama zake  (‘Alayhis Salaam).

 

Kwa hayo inakua wazi kuwa habari zilizokuja kuhimiza mut’a si maneno ya maimamu, isipokuwa nimaneno yaliyosemwa na watu kisha wakawasingizia maimamu  kwa kutaka kuwatusi AHLUL-BAYT,na kuwakosea adabu , na kama si hivyo itatafsiriwaje kuhalalisha kwao kufanya mut’a na familia ya Mtume na kuwaita makafiri wasiofanya mut’a?

Pamoja na kuwa maimamu wote (‘Alayhis Salaam) haikupatikana habari sahihi kuwa mmoja wao, aliwahi kufanya mut’a wala kuihalalisha mut’a, je  watakua wameishi  katika dini isiyo kuwa ya kiislamu?

Likiwa wazi kwetu hilo tutajua kuwa walioleta habari hizi ni wanafiki walio taka kuwatusi Ahlul-bait na maimamu (‘Alayhis Salaam), na kuzifanyia kazi habari hizi maana yake ni kuwakufurisha viongozi… basi zinduka.

Kulainy amepokea kutoka kwa Abii Abdillahi (‘Alayhis Salaam) kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Omar ibn Khatab akasema :hakika mimi nimezini akaamrisha kupingwa mawe,akaelezewa Amirul-muumini  (‘Alayhis Salaam) akamuuliza: vipi umezini? Akasema: nilipita kijijini ikanipata kiu kali sana nikamuomba maji bedui mmoja akakataa isipokua nitakapojitolea nafsi yangu kwake  (kukubali kuzini nae), ilipo nizidi kiu, nikahofia kufa akaninywesha maji nami nikamwachia nafsi yangu, akasema Amirul muumini (‘Alayhis Salaam) hiyo ni ndoa na apa kwa bwana wa Al kaaba, (AL FURU’U 2/193).

 

Hakika ya mut’a kama inavyojulikana  inakuwa kwa kuridhiana  pande mbili na kuwa na hamu baina yao, ama katika  upokezi huu mwanamke aliyetajwa alikuwa na shida, mwenye kulazimishwa,akajitolea nafsi yake ili apate kunywa maji, hii haichukuliwi ni zinaa kwa hiyo kulikuwa hakuna haja ya kutaka kutwaharishwa na ‘Umar , zaidi ya hayo -ni muhimu kuzingatia - kuwa  Amirul muuminin ndie ambae amepokea uharamu wa mut’a kwa kunakili toka kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika vita vya Khaybar,vipi atatoa fatwa hapa kuwa hii ni ndoa ya mut’a?! Na fatwa yake inaonyesha kuhalalisha kukubali na kuridhika  kwa kitendo cha mme na mke?!

Hakika fatwa hii lau angalisema mmoja wa wanafunzi ingehesabiwa  kwake ni kosa ambalo anstahiki lawama juu yake basi iweje kosa hili linasibishwe na Amiril-muminin (‘Alayhis Salaam)ambae anafahamika ni nani katika elimu na fatwa?

 

Hakika yule aliyeinasibisha fatwa hii kwa Amirul muuminina ama ni mwenye chuki anayetaka kumtukana, au ni mwenye lengo jengine kwa hiyo akazusha kisa hiki na kukinasbisha kwa Amirul-muminin ili aifanye mut’a iruhusike kisheria ili yeye na wenzake kama yeye waweze kujihalalisha zinaa kwa jina la dini, hata kwa gharama ya kuwasingizia maimamu bali hata kumsingizia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Na hakika uharibifu unaopatikana katika ndoa ya mut’a ni makubwa kwa pande tofauti: 

 1. Inapingana nasi (maelezo) ya kisheria kwa sababu ni kuhalalisha alicho kiharamisha Allah.

 

 1. Hakika limesababisha jambo hili (la kuhalalisha mut’a) kutengeneza riwaya za uongo na kuzinasibisha kwa maimamu (‘Alayhis Salaam) pamoja na matusi machafu yaliyomo ndani yake ambayo hawezi kuyaridhia yoyote yule mwenye imani japo chembe ndogo tu. 

 

 1. Na   miongoni mwa uharibifu wa mut’a  ni kuruhusu kufanya mut’a  na mwanamke aliye jihifadhi,aliyeolewa hata kama  yupo kwa mwanamme bila ya mmewe kujua, na katika hali hii  wanaume hawatakua na imani kwa wake zao, kwasababu inawezekana mwanamke kuolewa kwa mut’a bila mumewe wa kisheria  kufahamu na bila ridhaa yake;na huu ni uharibifu hakuna uharibifu zaidi ya huu.  Tazama (FURUU AL KAFIY 5/463), (TAHDHIYBUL-AL AHKAMI 7/554) - (AL- ISTIBSAAR 3/145).

  Yatakuaje mawazo yake tu na hisia zake siku atakapogundua kuwa mkewe ambae yupo katika himaya yake ameshaolewa  na mwanamume mwingine ndoa ya mut’a?!

 

 1. Na wazazi vilevile hawatakuwa na imani na mabinti zao wadogo kwa sababu wanaweza kuolewa ndoa ya mut’a bila wao kujua,  ni anaweza baba kustukizwa na uja uzito wa mwanae mdogo , …kwa nini… imekuaje…? hajui… ni ya nani ? Hajui pia aliolewa na mtu? Ni nani? Hakuna anaejua, kwa sababu alimuacha akaondoka zake.

 

 1. Watu wengi wanaofanya mut’a  wanajiruhusu wao kufanya mut’a na mabinti za watu,lakini wao watakapoendewa na mtu kwa ajili ya kuposa binti zao, au jamaa zao akitaka kuoa mut’a hawakubali na hawaridhiki ,kwa sababu wao wanaona  ndoa ya aina hii inafanana sana na zinaa, na kwa hiyo ni aibu kwao nao wanalihisi hilo  pale wanapo fanya mut’a na  na bint za watu, basi hakuna  shaka yakuwa wao wanajizuia  kuwaozesha mabinti zao kwa wengine ndoa ya mut’a maana yake  ni kuwa wana jihalalishia kufanya mut’a na mabinti za watu wakati wao wanawaharmishia watu kufanya mut’a na mabinti zao.

  Ikiwa mut’a imeruhusiwa kisheria au ni jambo la mubaha basi kwa nini kuna uzito wa kuwaruhusu wageni kufanya mut’a na mabinti zao au jamaa zao?!

 

 1. Hakika ndoa ya mut’a haina kushuhudiza wala kutangaza , wala kuridhia  walii wa mke wala hakuna kuridhiana , isipokuwa mut’a ni mkodisho tu,kama inavyo semekana kua Abuu abdillahi kasema hivyo, basi iweje jambo lenye picha kama hii litangazwe na kuenezwa kwa watu?

 

 1. Hakika ndoa ya mut’a imewafungulia mlango wanaume na wanawake wasiokuwa na maadili hasa vijana katika kuuengemeza uchafu wao kwa jina la dini , na limepelekea hilo kuiharibu sura ya dini na watu wake , kwa hiyo yanabainika madhara ya mut’a kidini kijamii na kitabia , na kwa sababu hiyo iliharamishwa mut’a, na kama mut’a ingekuwa na faida isinge haramishwa ,lakini ilipokuwa madhara yake ni makubwa Mtume aliiharamisha na Amiril-muminin pia akawa na msimamo huo.

 

Share