Mama Alimwachia Fedha Kwa Matumizi Ya Nyumbani, Mama Amefariki Je, Hizo Pesa Agawane Na Nduguze?

SWALI:

Asalam aleiykum.

Nimeishi na mamangu, aliniachia pesa, alfu thelathini. Pesa hizi aliniambia nizamatumizi hapa nyumbani, waweza kutumia hapa nyumbani. Sikutumia hizi alfu thelathini. Akafariki baada ya mwaka. Je nafaa ni gawanye hizi pesa na ndugu zangu? Ama haina haja ya kugawanya? Tuko ndugu saba, wa kiume wawili na wakike watano (nielezee kiwango cha kila mmoja wetu kama itabidi tugawanye)


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuachiwa pesa mama kwa ajili ya matumizi.

Hujatueleza kama mama yako alikuwekea sharti kama hukuzitumia fedha hizo utazirudisha?

Ikiwa mama aliweka sharti hilo itakuwa pesa hizo ni lazima uzigawe na warithi wenzako. Warithi wenzako ni ndugu zako, mumewe mama ikiwa yu hai na wazazi wake.

Ikiwa hakuna sharti lolote ila uliambiwa ni za matumizi tu hizo pesa zilikuwa ni zako kabla ya mama yako kufariki, na sasa pia ni zako peke yako kwa kupewa wewe na mama yako.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share