023-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Atakayemtimizia Haja Nduguye Na Kumsitiri Atapata Faraja Na Sitara Siku Ya Qiyaama

 Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 23

 Atakayemtimizia Haja Nduguye Na Kumsitiri Atapata Faraja Na Sitara Siku Ya Qiyaama

 

www.alhidaaya.com

 

 عن ابْنَ عُمَرَ (رضي الله عنهما)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ: ((الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لاَ يَظْلِمُهُ ولاَ يُسْلِمُهُ، وَمَنْ كَانَ فِي حَاجَةِ أَخِيهِ كَانَ اللَّهُ فِي حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً فَرَّجَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرُبَاتِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)  kwamba Rasuli  wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muislamu ni ndugu wa Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi [kwa adui]. Na atakayemtimizia haja nduguye, Allaah Atamtimizia haja yake. Na atakayemfariji [atakayemuondoshea] Muislamu dhiki yake, Allaah Atampa faraja ya dhiki zake Siku ya Qiyaamah. Na atakayemsitiri Muislamu mwenzake [aibu zake], Allaah Atamsitiri [aibu zake] Siku ya Qiyaamah)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Waislamu ni ndugu wanapasa kutendeana mema. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿١٠﴾

Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa. [Al-Hujuraat: 10]

 

Pia rejea: Al-Maaidah (5: 2).

Rejea pia Hadiyth namba (20), (21).

 

 

 

2. Uislamu unakataza kufanyiana dhulma.

 

Rejea Hadiyth namba (19).

 

Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema katika Hadiyth Qudsiy: ((Enyi waja Wangu! Mimi Nimejiharamishia dhuluma juu ya Nafsi Yangu na Nikaifanya ni haramu baina yenu basi msidhulumiane)). [Muslim]

 

 

3. Waislamu wanapasa kusaidiana dhidi ya adui.

 

 

4. Himizo la kusaidiana wakati wa dhiki na shida.

 

 

5. Himizo la kusitiriana aibu na onyo kali la kuieneza aibu, kashfa, uzushi n.k. kwa wengineo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٩﴾

Hakika wale wanaopenda uenee uchafu wa kashfa kwa wale walioamini; watapata adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na Allaah Anajua nanyi hamjui [An-Nuwr (24: 19)]

         

 

6. Malipo ya Aakhirah ni makubwa zaidi kuliko ya duniani. Rejea An-Nahl (16: 41).

 

 

7. Rahma ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuwalipa waja wanapotendeana wema.  

 

 

8. Muislamu akhiari kumwondoshea dhiki nduguye duniani apate kuondoshewa dhiki Siku ya Qiyaamah, kwani huko ndiko kwenye dhiki na shida kubwa zaidi.

 

Rejea: Al-Hajj (22: 1-2).

 

 

Share