105-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Allaah Atawatesa Watesao Watu Duniani

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 105

 

Allaah Atawatesa Watesao Watu Duniani

 

 

 

 

عَنْ هِشَامُ بْنُ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ (رضي الله عنهما) أنّهُ  مَرَّ بِالشَّامِ عَلَى أُنَاسٍ وَقَدْ أُقِيمُوا فِي الشَّمْسِ وَصُبَّ عَلَى رُءُوسِهِمْ الزَّيْتُ فَقَالَ: مَا هَذَا؟ قِيلَ: يُعَذَّبُونَ فِي الْخَرَاجِ،  فَقَالَ: أَشْهَدُ لَسمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((إِنَّ اللَّهَ يُعَذِّبُ الَّذِينَ يُعَذِّبُونَ النَّاسَ  فِي الدُّنْيَا)) فَدَخَلَ على الأمِيرِ، فَحَدَّثَهُ فأمَرَ بِهِمْ فَخلوا – رواه مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Hishaam bin Hakiym bin Hizaam (رضي الله عنهما) kwamba aliwapitia watu Shaam waliosimamishwa juani na kumwagiwa mafuta vichwani mwao. Akasema: Nini hii? Ikasemwa: “Wanateswa sababu ya kutokulipa kodi”. Akasema: “Nashuhudia hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Allaah Atawatesa wanaowatesa watu duniani)). Akaingia kwa Amiyr, akamwelezea, akawaamrisha, wakaacha. [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Kushindwa kulipa kodi au gharama zozote kusiwe ni sababu ya kuwatesa watu, bali inapasa mwenye wasaa afikirie hali ya Muislamu mwenzake na ashirikiane naye kwa kila njia kumsahilishia hali yake, kama kumpa muda wa kulipa deni lake au kumsamehe. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾

Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkifanya deni kuwa ni swadaqah basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua.  [Al-Baqarah (2: 280)].

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢

Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu. [Al-Maaidah: 2]

 

 

2. Tisho la kuwaadhibu watu waliodhaifu, maskini bila ya haki.

 

 

3. Hima ya Maswahaba kuamrisha mema na kukataza maovu, na hiyo ni amri kwa Waumini wote.

 

Rejea: Aal-‘Imraan (3: 104, 110), At-Tawbah (9: 71, 112), Al-Hajj (22: 41).

Pia Hadiyth: Imepokewa kwa Jariyr bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) kuwa alimbai Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah na kumnasihi kila Muislamu.. [Musim]

 

 

4. Waislamu wanapaswa kuoneana huruma pindi wanapoona ndugu zao wanateswa, na wafanye hima kuwaokoa katika mateso.

 

Rejea Al-Fat-h (48: 29).

 

 

5. Tahadharisho la madhalimu kutokana na dhulma.

 

Rejea Hadiyth namba (19), (93).  

 

 

 

Share