107-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Anayeirejelea Hiba Yake Ni Kama Mbwa Anayerudia Matapishi Yake

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 107  

 

Anayeirejelea Hiba Yake Ni Kama Mbwa Anayerudia Matapishi Yake

 

 

 

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما)  أَنَّ رَسُولَ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((الَّذِي يَعُودُ فِي هِبَتِهِ كَالْكَلْبِ يَرْجِعُ فِي قَيْئِهِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)   kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Anayeirudia hiba yake ni kama mbwa anayerudia matapishi yake)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Makatazo ya kukirudia (kukichukua tena) kitu alichokitoa mtu kama zawadi n.k.

 

 

2. Kupeana zawadi, hiba n.k. kunajenga mapenzi baina ya ndugu, hivyo anapoirudia au anapoidai hiba alioitoa, italeta madhara ya kubomoa mapenzi yaliyoko baina ya ndugu hao.

 

Hadiyth: ((Peaneni zawadi mtapendana)). [Imaam Maalik katika al-Muwattwaa’ na Atw-Twabaraaniy katika Al-Awsatw]

 

 

3. Uislamu unazuia kila aina za maudhi baina ya watu.

 

 

4. Mfano wa vilotajwa; mbwa na matapishi, vyote ni vitu vichafu. Hii ni dalili jinsi gani uovu wa kufanya jambo hilo, kwamba hiba imefananishwa na matapishi, na mbwa amefananishwa na mtu anayerudia hiba yake.

 

 

5. Kupeana zawadi ni miongoni mwa ‘amali njema atakazokuta malipo yake mtu Siku ya Qiyaamah, kwa hiyo asitamani kukirudia anachokitoa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى): 

 

 وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ

Na chochote kile cha kheri mnachokadimisha kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Allaah. Ni bora, na ujira mkubwa zaidi. [Al-Muzzammil: 20]

 

Na rejea pia:  Aal-‘Imraan (3: 92), Sabaa (34: 39)

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى): 

 

وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١٠﴾

na lolote mnalolitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu katika kheri mtalikuta kwa Allaah, hakika Allaah kwa yale myafanyao ni Mwenye kuona. [Al-Baqarah (2: 110)]

 

 

 

 

 

 

Share