Qur-aan Ama 'Aqiydah; Ipi Ije Mwanzo?

 

Qur-aan Ama 'Aqiydah; Ipi Ije Mwanzo?

 

Imefasiriwa Na: Abuu 'Abdir-Rahmaan

 

Alhidaaya.com

 

Imesemwa katika mwendo wa Maswahaba na Sunnah, ni kuwa walikuwa wakiwafundisha watoto kwanza Tawhiyd (Elimu ya kumpwekesha Allaah) kabla ya Qur-aan, kinyume na sasa.

Imesimuliwa na Ibn Maajah na akaisahihisha Al-Albaaniy kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Umar  (Allah awe radhin nao) amesema:
"
Cha mwanzo tulichokuwa tukifundishwa, ilikuwa 'Aqiydah kwanza kabla ya Qur-aan na tulikuwa tunafundishwa Aayah zinokataza jambo ama kuhimiza jambo. Na nimeona wanafunzi wengi waliosoma Qur-aan kabla ya elimu ya 'Aqiydah, anasoma mwanzo wa Msahafu mpaka mwisho lakini haelewi nini Qur-aan inaamrisha ama nini inakataza, na ni msimamo upi anapaswa kuwa nao kuhusiana na hicho, ni sawa na mtu amekaa kisha anazitupa tende; yaani, hanufaiki na usomaji wake."

 

Na katika masimulizi mengine ya Al-Bayhaqiy na Al-Haakim ambaye amesahihisha masimulizi hayo, ni kuwa Ibn Al-Qayyim alisema:

"Wakifikia (watoto) wakati wa kuanza kuzungumza, wafanye watamke Laa Ilaaha Illa Allaah, Muhammad Rasuwl-Allaah, nalo liwe ni jambo la mwanzo linagonga katika masikio yao, kumjua Allaah Aliyetukuka, kujua Tawhiyd kumhusu Allaah, na kwamba Yeye (Allaah) Yupo juu ya 'Arsh Yake, na kwamba Anawaona (Waja Wake), na Anawasikia wanayozungumza, na kwamba Yeye yupo nao popote walipo (kwa elimu Yake)..."

 

Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab aliandika risala akaiita "Kuwafundisha Watoto Tawhiyd', alieleza katuika utangulizi wake:

 

"Risala hii ni yenye manufaa inayoonesha uwajibu wa kuwafundisha watoto (Tawhiyd) kabla ya kuwafundisha wao Qur-aan. Kwa hali hiyo, mtoto ananyunyukia na kuwa ni mtu aliyekamilika mwenye Fitwrah ya ki-Islamu kamili chini ya Tawhiyd."

 

Na kama ilivyoulizwa vilevile:

"Je, tuanze kujifundishe kile ambacho ni Waajib kama vile Swalah, Swawm na Twahaarah? Au tuanze na kuhifadhi Qur-aan? 

Ibn Mubaarak akajibu:

Kama unayo yenye kukutosha katika Qur-aan cha kukuwezesha kusoma pindi unaposwali, basi katafute elimu."

 

Nasema, kwa sababu kutafuta elimu ya Dini ni Waajib na kuhifadhi Qur-aan ni Mustahab (Jambo lenye kupendekezwa), hivyo huwezi kutanguliza la Mustahab na kuliacha la Waajib.

 

 

Share