02-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Inahusiana Na Majina Mazuri Ya Allaah Na Sifa Zake

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

02-Tawhiyd Inahusiana Na Majina Mazuri Ya Allaah Na Sifa Zake

 

 

 

 

Tawhiyd inahusiana na Majina Mazuri ya Allaah na Sifa Zake.  Ndio maana Aayatul Kursiyy ikawa ni Aayah bora kabisa katika Qur-aan na Suwratul-Ikhlaasw ikawa thawabu zake kuisoma ni sawa na thuluthi ya Qur-aan kwa sababu ndani yake zinaelezea Majina na Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah: 255]

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee.

 

اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾

 “Allaah ni Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote. 

 

 

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾

 “Hakuzaa na wala Hakuzaliwa.

 

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾

 “Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”  [Ikhlaasw: 112]

 

 

Share