13-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Kauli Ya Tawhiyd Ndio Bora Kabisa Waliyotamka Rusuli Wote

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

13-Kauli Ya Tawhiyd Ndio Bora Kabisa Waliyotamka Rusuli Wote

 

 

Imepokelewa kutoka kwa babu yake ‘Amru bin Shu’ayb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema:

 

((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ, وَخَيْرُ مَا قُلْتُ أَنَا وَالنَّبِيُّونَ مِنْ قَبْلِي: لَا إِلَهَ إِلَّااللَّهُوَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ))

((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:  “Laa Ilaaha Illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr” [Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Peke Yake, Hana mshirika. Yeye Ndiye Mwenye Ufalme na Ndiye Mwenye kuhimidiwa, Naye ni Muweza wa kila kitu])). [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy 3585]

 

 

Neno la Tawhiyd ni dhikri (utajo) bora kabisa:

 

 عن جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ يَقُولُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "أَفْضَلُ الذّكْر لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ الْحَمْدُ لِلَّهِ"

Kutoka kwa Jaabir bin ‘AbdiLLaah amesema: “Nimesmikia Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Dhikri bora kabisa ni “laa ilaaha illa Allaah”, na du’aa bora kabisa ni “AlhamduliLLaah”)). [At-Tirmdhiy na Ibn Maajah].

 

 

Na ndio maana Aayah tukufu kabisa ikawa ni Aayatul-Kursiyy (Al-Baqarah 2: 255) na Suwratul-Ikhlaasw (112) ikawa ni sawa na thuluthi ya Qur-aan, japokuwa ni Suwrah ndogo kabisa.

 

 

 

Share