Hiwsnul-Muslim: Utangulizi Wa Mwandishi

Hiwsnul Muslim

Utangulizi Wa Mwandishi

www.alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم

 

Hakika Himdi ni za Allaah, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunajikinga kwa Allaah kutokana na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemhidi Allaah hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa kumhidi. Nashuhudia kwamba, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, Hana mshirika, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Rasuli Wake. Rahmah na amani zimfikie pamoja na ahli zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka Siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.

 

 

Baada ya yaliyotangulia huu ni mukhtasari wa kitabu changu kiitwacho Hiswnul-Muslim min Adhkaaril-Kitaabi was-Sunnah.

 

Ninamuomba Allaah عزَّوجلَّ kwa Majina Yake mazuri, na Sifa Zake zilizotukuka, Ajaaliye kazi hii yenye ikhlaasw kwa ajili ya Radhi Zake, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukisambaza, hakika Yeye Allaah سبحانه Ndiye  Mlinzi na Muweza.

 

Rahmah na amani zimfikie Nabiy wetu  Muhammad na ahli zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.

 

 

 

Share