Halawiyaat Za Tambi Za Kukaanga Kwa Lozi Na Zabibu

Halawiyaat Za Tambi Za Kukaanga Kwa Lozi Na Zabibu

Vipimo
Tambi nyembamba za brown - 2 paket
Siagi - 4 Vijiko vya supu
Maziwa mazito (condensed milk) - 300 ml
Lozi zilomenywa na kukatwa nyembamba - 1 kikombe
Zabibu kavu - 1 kikombe
Arki ya rosi (rose essence) - 1 kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka karai katika moto tia siagi iyayuke
  2. Vunjavunja tambi kisha zikaange bila ya kuachia mkono, mpaka zigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
  3. Tia lozi na zabibu
  4. Tia maziwa mzito (condensed milk) na arki ya rosi endelea kuchanganya
  5. Zima jiko kisha teka kikombe kidogo cha kahawa ya Kiarabu ujaze nusu ya kikombe.
  6. Weka katika sahani nzuri ya kupakulia
  7. Endelea kuteka na kuweka katika sahani mpaka mchanganyiko umalizike.

 

Share