41-Kitaab At-Tawhiyd: Ni Kufuru Kukanusha Neema Ya Allaah Baada Ya Kuitambua

Mlango Wa 41

باب:  يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللَّـهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ

Ni Kufuru Kukanusha Neema Ya Allaah Baada Ya Kuitambua

 


 

 

 قَوْلُ اللَّهِ تَعَالَى:

Kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللَّـهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٣﴾

((Wanazijua neema za Allaah, kisha wanazikanusha; na wengi wao ni makafiri)) [An-Nahl: (16: 83)]

 

  قَالَ مُجَاهِد مَا مَعْنَاهُ: هُوَ قَوْلُ الرَّجُلِ هَذَا مَالِي، وَرِثْتُهُ عَنْ آبَائِي

Mujaahid kasema: “Maana yake ni: Mtu kusema: Hii mali yangu nimeirithi kwa baba zangu.

 

وَقَالَ عَوْنُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ: يَقُولُونَ لَوْلا فُلانٌ لَمْ يَكُنْ كَذَا

Na ‘Awn bin ‘Abdillaah amesema: “Wanasema lau kama si fulani, isingelikuwa hivi! (hizo neema, na hali wanajua kwamba Allaah Ndiye Anayetoa uwezo na tawfiq).”

 

وَقَالَ اِبْنُ قُتَيْبَةَ يَقُولُونَ: هَذَا بِشَفَاعَةِ آلِهَتِنَا

Na Ibn Qutaybah kasema: “Wanasema hizi (neema) ni kutokana na shafaa’ah (uombezi) wa waabudiwa wetu”

 

وَقَالَ أَبُو الْعَبَّاسِ بَعْدَ حَدِيثِ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الَّذِي فِيهِ وَأَنَّ اللهَ تَعَالَى قَال: ((أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ)) الْحَدِيثِ، وَقَدْ تَقَدَّمَ: وَهَذَا كَثِيرٌ فِي الْكِتَابِ وَالسُّنَّةِ، يَذُمُّ سُبْحَانَهُ مَنْ يُضِيفُ إِنْعَامَهُ إِلَى غَيْرِهِ وَيُشْرِكُ بِهِ.

Na Abuu Al-‘Abbaas (Ibn Taymiyyah) kasema baada ya Hadiyth ya Khaalid ambayo humo Allaah Ta’aalaa Amesema: ((Baadhi ya waja Wangu wameamka leo wakiwa wenye kuniamini, na wengine wamekufuru)) [Hadiyth imetangulia][1]. Na amri hizi ni nyingi katika Qur-aan na Sunnah. Allaah Anashutumu anayeegemeza neema (na rahmah) Zake kwa wengine na wanaomshirikisha Naye.

 

قَالَ بَعْضُ السَّلَفِ: هُوَ كَقَوْلِهِمْ: كَانَتِ الرِّيحُ طَيِّبَةً، وَالْمَلاَّحُ حَاذِقًا.. وَنَحْوَ ذَلِكَ مِمَّا هُوَ جَارٍ عَلَى أَلْسِنَةٍ كَثِيرَةٍ

Na baadhi ya Salaf wamesema: Ni kauli zao: “Upepo ulikuwa mzuri.” Na “Nahodha alikuwa hodari (na hali wanajua aliyewafikisha salama ni Allaah na si uzuri wa upepo wala uhodari wa nahodha) na mfano wa maneno kama hayo yanayosemwa na watu wengi.

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Maelezo kuhusu neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kisha ukanushaji wake.

 

2-Watu wengi wayasema hayo (kukanusha neema za Allaah).

 

3-Kutaja kauli hizo ni sawa na kukanusha neema za Allaah.

 

4-Kujumuisha moyoni mambo mawili yenye kupingana; kama kuitambua neema ya Allaah (سبحانه وتعالى) kisha kuzikanusha.

 

 

[1]  Taz. Mlango Wa 30.

 

 

Share