208-Aayah Na Mafunzo: Hatua Za Shaytwaan Na Fadhila Za Kutokumfuata

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

www.alhidaaya.com

 

Hatua Za Shaytwaan Na Fadhila Za Kutokumfuata

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾

208. Enyi walioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

 

 

Mafunzo:

عَنْ سَبْرَةَ بْنِ أَبِي فَاكِهٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((إِنَّ الشَّيْطَانَ قَعَدَ لاِبْنِ آدَمَ بِأَطْرُقِهِ ، فَقَعَدَ لَهُ بِطَرِيقِ الإِسْلاَمِ فَقَالَ: تُسْلِمُ وَتَذَرُ دِينَكَ وَدِينَ آبَائِكَ وَآبَاءِ أَبِيكَ؟ فَعَصَاهُ فَأَسْلَمَ ، ثُمَّ قَعَدَ لَهُ بِطَرِيقِ الْهِجْرَةِ فَقَالَ: تُهَاجِرُ وَتَدَعُ أَرْضَكَ وَسَمَاءَكَ؟ وَإِنَّمَا مَثَلُ الْمُهَاجِرِ كَمَثَلِ الْفَرَسِ فِي الطِّوَلِ،  فَعَصَاهُ فَهَاجَرَ، ثُمَّ قَعَدَ لَهُ بِطَرِيقِ الْجِهَادِ فَقَالَ: تُجَاهِدُ فَهُوَ جَهْدُ النَّفْسِ وَالْمَالِ فَتُقَاتِلُ فَتُقْتَلُ فَتُنْكَحُ الْمَرْأَةُ وَيُقْسَمُ الْمَالُ؟ فَعَصَاهُ فَجَاهَدَ‏)) ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : ((فَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ ،  وَمَنْ قُتِلَ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ ،  وَإِنْ غَرِقَ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ ، أَوْ وَقَصَتْهُ دَابَّتُهُ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ))‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Sabrah bin Abiy Faakih (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika shaytwaan humkalia mwana Aadam katika njia zake. Humkalia katika njia ya Islaam husema: “Hivi utaingia katika Uislamu uache dini  yako na dini ya baba yako na ya babu zako?” Lakini akamuasi akasilimu. Kisha akamkalia njia ya hijrah. Akasema: “Hivi utahajiri uache nchi yako na mbingu zake? Hakika mwenye kuhajiri ni kama farasi aliyefungwa kwenye kigingi.” Lakini akamuasi akahajiri. Kisha akamkalia njia ya jihaad akasema: “Hivi utapigana jihaad ugharimu uhai wako na mali yako. Utapigana na utauliwa, na mkeo ataolewa na mali yako itagawanywa.” Lakini akamuasi akapigana jihaad)) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Atakayefanya hivyo atakuwa na haki kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) Amuingize Jannah. Na atakayeuliwa atakuwa na haki kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) Amiuingize Jannah. Atakayezama atakuwa na haki kwa Allaah Amuingize Jannah. Atakayeangushwa na mnyama wake akavunjika shingo, atakuwa na haki kwa Allaah Amuingize Jannah)).

 

[An-Nasaaiy – Kitaab Al-Jihaad na ameisahihisha Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika Swahiyh An-Nasaaiy (3134), na taz. Swahiyh Al-Jaami’ (1652)]

Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: “Kila Alichokiharamisha Allaah (Ta’aalaa) ni katika hatua za shaytwaan, ikiwa ni kutakabari, au kuongopa, au isthzai au mengineo, kwa sababu huyaamrisha na huyaitia na huyalingania.” [Tafsiyr Al-Faatihah wal Baqarah (2/234)]  

 

 

Share