245-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Kwa Ajili Ya Allaah Ni Kuzidishwa Mali Na Fadhila Tele Nyenginezo

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kutoa Kwa Ajili Ya Allaah Ni Kuzidishwa Mali Na Fadhila Tele Nyenginezo

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾

245. Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa.

 

 

Fadhila tele zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah kuhusu kutoa mali katika njia ya Allaah; miongoni mwazo ni

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ  وَمَا زَادَ اللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إلاَّ عِزًّا  وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلاَّ رَفَعَهُ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ)) مسلم        

  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kutoa swadaqah hakupunguzi mali, Allaah Humzidishia mja ‘izzah (utukufu) kwa ajili ya kusamehe kwake.  Na   yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah, Allaah (عزّ وجلّ) Atampandisha Daraja [Atamtukuza] [Muslim]

 

 

 

Pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا مِنْ يَوْمٍ يُصْبِحُ الْعِبَادُ فِيهِ إلاَّ مَلَكَانِ يَنْزِلاَنِ فَيَقُولُ أَحَدُهُمَا: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُنْفِقًا خَلَفًا. وَيَقُولُ الأَخَرُ: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُمْسِكًا تَلَفًا)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila siku inayowapambaukia watu kuna Malaika wawili wanateremka, mmoja wao akiomba: Ee Allaah! Mwenye kutoa [sadaka] mlipe zaidi. Na mwengine huomba: Ee Allaah! Mwenye kuzuia mpe hasara)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share