262-Aayah Na Mafunzo: Anayesimbulia Alichotoa Hatotazamwa Na Allaah Siku Ya Qiyaamah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Anayesimbulia Alichotoa Hatotazamwa Na Allaah Siku Ya Qiyaamah

 

 

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾

262. Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

 

Mafunzo:

 

 

Abuu Dharr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu watatu Allaah Hatowazungumzisha Siku ya Qiyaamah, wala Hatowatazama, wala Hatowatakasa, na watapata adhabu inayoumiza.” Akayakariri maneno hayo mara tatu. Abuu Dharr akasema: Wamepita patupu na wamekhasirika! Ni nani hao Ee Rasuli wa Allaah?  Akasema: “Al-Musbil (mwenye kuburuza nguo yake), mwenye kutoa kisha akasimbulia alichokitoa, na mwenye kuuza bidhaa zake kwa kutumia kiapo cha uongo.” [Muslim]

 

 

 

Share