272-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Swadaqah Kutaraji Wajihi Wa Allaah Ni Kupandishwa Daraja

 

 

Al-Baqarah

Kutoa Swadaqah Kutaraji Wajihi Wa Allaah Ni Kupandishwa Daraja

 Alhidaaya.com 

 

لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye. Na chochote cha kheri mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.

Mafunzo:

 

Fadhila za kutoka swadaqah: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia Sa’d bin Abiy Waqaasw (رضي الله عنه) alipomzuru mgonjwa (na mapokezi mengine alipokuwa Hijjatul-Widaa’): “Hutatoa swadaqah na huku ukitarajia Wajihi wa Allaah ila utapanda daraja ya juu kwa sababu yake ikiwa ni pamoja na kile unachokitoa kwenye kinywa cha mkeo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share