007-Aayah Na Mafunzo: Halaal Na Haraam Imebainika Baina Yake Ni Yenye Shubha

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Halaal Na Haraam Imebainika Baina Yake Ni Yenye Shubha

www.alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧

7. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu) na kutafuta maana zake zilofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu.” Na hawakumbuki ila wenye akili

 

Mafunzo:

 

Aayaat Muhkamaat: Ni Aayaat ambazo maana zake zinafahamika kiwepesi, hazina mushkila wala utata, na dalili zake ziko wazi. 

 

Aayaat Mutashaabihaat: Ni Aayah ambazo ni ngumu kufahamika, na zinawatatanisha baadhi ya watu wasio na ‘ilmu ya kutosha

 

 

Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliisoma Aayah hii: “Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu …” mpaka mwisho wa Aayah, kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Ee ‘Aaishah! Pindi utakapowaona wale ambao wanafuata zile Aayaat ambazo haziko wazi zaidi, basi fahamu kuwa hao ndio wale ambao Allaah Amewataja katika hii Aayah, basi tahadharini nao.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Na pia,

 

عَن النُّعْمَانَ بْنَ بَشِيرٍ (رضي الله عنهما) قَال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:  ((الْحَلاَلُ بَيِّنٌ وَالْحَرَامُ بَيِّنٌ, وَبَيْنَهُمَا مُتَشَابِهَاتٌ لاَ يَعْلَمُهَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ, فَمَنْ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ اسْتَبْرَأَ  لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ,  وَمَنْ وَقَعَ فِي الشُّبُهَاتِ وَقَعَ فِي الْحَرَامِ,  كَالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى َيُوشِكُ أَنْ يَرْتَعْ فِيهِ, أَلاَ وَإِنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى,  أَلاَ وَإِنَّ حِمَى اللَّهِ مَحَارِمُهُ, أَلاَ وَإِنَّ فِي الْجَسَدِ مُضْغَةً إِذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّه, وَإِذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ أَلاَ وَهِيَ الْقَلْبُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakika halali iko wazi na haramu iko wazi. Baina ya mawili hayo mna yenye kutia shaka. Wengi miongoni mwa watu hawayajui. Basi atakayejiepusha yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake. Na Atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye haramu. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha humo [mpaka mwingine wa watu]. Zindukeni!  Kila mfalme ana mipaka. Zindukeni! Kwa yakini mipaka ya Allaah ni haramu Alizoziharamisha. Zindukeni! Kwa yakini katika mwili mna kinofu [cha nyama], kinapokuwa sahihi, mwili wote unakuwa sahihi. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Zindukeni! Kinofu hicho ni moyo)). [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Share