113-Aayah Na Mafunzo: Sababu Ya Kuteremka Hawako Sawasawa Ahlil-Kitaab

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Sababu Ya Kuteremka Hawako Sawasawa Ahlil-Kitaab  

  

 

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

114. Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza munkari na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Swalihina.

 

وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾

115. Na kheri yoyote waifanyayo hawatokanushiwa (thawabu zake).  Na Allaah ni Mjuzi wa wenye taqwa.

Mafunzo:

 

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba: (Siku moja) Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) aliichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa kisha akatoka kuja kuiswali Masjid akawakuta Maswahaba  (رضي الله عنهم)vado wamemsubiri akasema: “Uhakika wa mambo ulivyo hakuna yoyote katika Watu wa Dini hizi anayemdhukuru Allaah katika wakati huu asiyekuwa nyinyi.” Hapo ikateremka Aayah: Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi…” mpaka mwisho wa Aayah 115. [Hadiyth ya Ibn Mas’uwd ameipokea Al-Imaam Ahmad].

 

 

 

Share