134-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Anayezuia Ghadhabu

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Anayezuia Ghadhabu

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:)

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾ 

Ambao wanatoa (kwa ajili ya Allaah) katika hali ya wasaa na katika hali ya shida, na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. [Aal-'Imraan: 134]

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Aliye na nguvu si mwenye kushinda katika mieleka lakini mwenye nguvu ni ambaye anazuia nafsi yake kutokana na ghadhabu.” [Imaam Ahmad].

 

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayezuia ghadhabu zake hali ya kuwa anaweza kuzidhihirisha, Allaah Atamwita huku wakishuhudia viumbe wote mpaka Ampe chaguo la Huwr (wanawake wazuri Jannah wenye macho mazuri) wowote awatakao.” [Ahmad].

 

 

 

Share