200-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Ribaatw Fiy SabiliLLaah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Ribaatw  Fiy SabiliLLaah

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾

200. Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.

 

Mafunzo:

 

Baadhi Ya Maana Ya Ribaatw Na Fadhila Zake:

 

Kwanza:  Kubakia, kuthibitika kuchunga, kulinda mipaka katika Jihaad fiy SabiliLLaah

 

Pili:          Kubakia katika ‘Ibaadah baina ya Swalaah Na Swalaah ya pili.

 

Fadhila za Ribaatw:

 

Sahl bin Sa’ad (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ar-Ribaatw (kuthibitika katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) siku moja kwa ajili ya Allaah ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na sehemu ndogo katika Jannah (Peponi), kiasi cha ukubwa wa fimbo ya mmoja wenu, ni bora kuliko dunia na yaliyokuwemo ndani yake. Na safari ya asubuhi au ya jioni anayosafiri mja katika Njia ya Allaah ni bora kuliko dunia na vilivyomo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia:  Amesimulia Salmaan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ribaatw (kuthibitika katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja na usiku wake ni bora (katika malipo) kuliko Swiyaam ya mwezi mzima na Qiyaam (kisimamo cha kuswali usiku) chake. Na mtu akifariki (akiwa katika ribaatw), ‘amali zake zitaendelea kuandikwa na riziki yake ataendela kupata na atasalimika na fitnah (za kaburi).”  [Muslim].

 

 

Share