024-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 024: وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa     024-Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa...

 

 

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni shariy’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya yaliyowajibika. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kuhusu Maswahaba (رضي الله عنهم) , kwani wao siku ya Awtwaas (eneo lilipo baina ya Makkah na Twaaif ambapo walipatikana mateka baada ya vita vya Hunayn mwaka wa 8 Hijriyyah) walipata wanawake ambao ni mateka, basi wakaona uzito kuwaingilia kwa sababu waume zao ni washirikina. Allaah  (عزّ وجلّ) Akateremsha Aayah hii:

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ  

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.

 

[Amehadithia Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه)  na imepokelewa na Muslim]

 

 

Share