127-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 127: وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

An-Nisaa  127-Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake.

 

 

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا ﴿١٢٧﴾

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa, na kuhusu wanaokandamizwa miongoni mwa watoto, na wajibu ulio juu yenu wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu. Na lolote mlifanyalo katika la khayr basi hakika Allaah daima kwa hilo Ni Mjuzi. (4:127).

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii inamzungumzia bwana mmoja aliyekuwa anamlea bint yatima na alikuwa ni msimamizi na mrithi wake.  Amehadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ  

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa. (4:127),  

 

imeteremshwa kuhusu kesi ya bwana aliyekuwa anamlea bint yatima. Bwana huyo alikuwa ni msimamzi wake na mrithi wake. Yatima huyo alishirikiana naye katika mali ya huyo bwana mpaka katika (shamba la) mtende. Mlezi huyo akawa na raghba ya kumuoa yatima (juu ya kuwa hakumpenda) na hakupenda kumuozesha mtu mwengine asije kushirikiana naye mali yake (ya yatima) ambayo anashirikiana naye. Na kwa sababu hii, mlezi huyo alimzuia yatima huyo kuolewa, na hapo ikateremshwa Aayah hii (4:127) na inayofuatia (4:128):

 

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ  

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa.

 

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:127-128).

 

[Al-Bukhaariy]

 

 

Katika riwaayah nyengine, ‘Urwah alimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها)  kuhusu Aayah:

 

 وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:128).

 

 

Aaishah (رضي الله عنها)   akahadithia kisa kama hicho cha bint yatima kwa nyongeza kuwa huyo bwana mlezi alitaka kumuoa kwa mahari kidogo kabisa kuliko walivyokuwa wakipewa wanawake wengine walio kama hali yake. Kisha watu wakaenda kutafuta fatwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ndipo Allaah Akateremsha Aayah:

 

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ  

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa. (4:127).  

 

 

[Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Dhulma Waliyokuwa Wakifanyiwa Mayatima Zama Za Jaahiliyyah:

 

 

‘Aliy bin Abiy Twalhah amesema: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Ilikuwa wakati wa  jaahiliyyah, mlezi wa yatima humfunga kamba binti yatima, hapo huwa hakuna ruhusa mtu kumuoa. Akiwa mzuri na akapenda kumuoa anamuoa na kudhibiti mali yake. Akiwa si mzuri, basi hamruhusu aolewe mpaka afariki, na akifariki yeye hurithi mali yake. Allaah Akaharamisha hili Akasema:

 

وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ  

Na kuhusu wanaokandamizwa miongoni mwa watoto, na wajibu ulio juu yenu wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu. (4:127).

  

 

Share