016-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto, Du'aa Yenye Jina Tukufu La Allaah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto

 

Du'aa Yenye Jina Tukufu La Allaah Ambalo Ukiomba Utakabaliwa

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَمْدَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ وَحْدَكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ الْمَنَّانُ يَا بَدِيعَ السَّمَوَاتِ وَالأرْضِ يَا ذَا الْجَلالِ وَالإكْرَامِ يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ

 

Allaahumma inniy as-aluka bianna lakal-hamdu laa ilaaha illa Anta Wahdaka laa shariyka Laka, Al-Mannaanu  yaa  Badiy-’as-samaawati wal-ardhwi, yaa dhal-Jalaali wal-ikraami, yaa Hayyu yaa Qayyuwmu, inniy as-alukal-Jannata wa a’uwdhu bika minan-naari

 

Ee Allaah, nakuomba, hakika kuhimidiwa ni Kwako hapana muabudiwa wa haki ila Wewe, Peke Yako Huna mshirika, Mwenye Fadhila. Ee Mwanzishi wa mbingu na ardhi ee Mwenye Utukufu na Ukarimu, ee Aliye Hai [daima], ee Msimamizi wa yote, hakika mimi nakuomba Jannah na najikinga kwako na moto.

 

Du’aa hii tukufu ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo amesema: baada ya mtu kuomba du’aa hii:

 

“Kwa yakini amemuomba Allaah kwa Jina Lake Tukufu Ambalo Anapoombwa kwalo Anaitikia na Anapotakwa kwalo jambo hutoa:

 

[Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhiywa Allaahu ‘anhu) - Abuu Daawuwd [1495], An-Nasaaiy (3/52), Ibn Maajah [3858] na taz. Swahiyh Ibn Maajah (2/329)]

 

 

Share