Nini Tofauti Ya Qiyaamul-Layl Na Swalaah Ya Taraawiyh?

Nini Tofauti Ya Qiyaamul-Layl Na Swalaah Ya Taraawiyh

 

SWALI:

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakatuhu.  Nataka kujua tofauti baina ya Swalah ya  Qiyaamul-Llay  na Swalah ya Tarawiy? Nitashukuru kupata jibu.  Jazakallah. Wassalamu alaikum warahmatullahi wabarakatuh.

 

 

JIBU:

AlhamduliLlaah.

Swalaah ya Taraawiyh ni Qiyaamul-Layl (kisimamo cha usiku). 

Hakuna tofauti baina ya Swalaah hizi mbili, kama watu wengi wanavyodhania.

 

Taraawiyh (mapumziko) imeitwa hivyo kwa sababu Salafus-Swaalih (wema waliotangulia (Allaah Awarehemu) walikuwa wakipumzika kila baada ya Rakaa mbili kwa sababu walifanya Swalaah zao kuwa ndefu ili kuchuma thawabu nyingi zilizoko katika msimu huu. 

 

Walikuwa wana hamu ya kuchuma thawabu zilizotajwa katika Hadiyth: ((Yeyote atakayesimama na kuswali usiku katika Ramadhawan kwa iymaan na kutarajia malipo, atafutiwa dhambi zake zote)) [imesimuliwa na Al-Bukhaariy No. 36]

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share