03-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Aliyepatwa Na Damu Ya Hedhi Baada Ya Kutiya Niyyah Ya Swawm

Aliyepatwa Na Damu Ya Hedhi Baada Ya Kutiya Niyyah Ya Swawm

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya mwanamke imemjia damu baada ya kutia niyyah ya swiyaam?

 

 

JIBU:

 

Ikiwa amefunga kisha ikamtokea damu ya mwezi, basi swawm yake imeharibika na inambidi afungue na ale masiku ya hedhi. Itakapokatika damu pindi imemalizika hedhi yake, basi arudie kufunga mwezi uliobakia kisha alipe masiku aliyokuwa hakufunga ambayo ni ya siku za hedhi yake.

 

 

[Al-Muntaqaa Min Fataawaa Al-Fawzaaan (7/51]

 

 

Share