Tambi Za Mchele Za Nazi Na Maziwa

Tambi Za Mchele Za Nazi Na  Maziwa

 

Vipimo

 

Tambi Za Mchele  paketi 1

Tui la nazi kikombe 1

Maziwa mazito kiasi tumia ya kopo, kikombe 1

Sukari ¾ kikombe

Samli ¼ kikombe

Zabibu kiasi

Arki (rose flavour) 1 kijiko cha chai

Hiliki ½ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

  1. Chemsha tambi ziwive kiasi tu, chuja maji
  2. Katika sufuria changanya vitu vyote ukoroge katika moto kisha mimina tambi.
  3. Changanya vizuri katika moto kiasi dakika 1 tu kisha mimina katika chombo cha kupikia katika oven (Oven proof) ubanike  (bake) kwa moto wa kiasi takriban dakika 20.
  4. Epua zikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

 

 

Share