05-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayesema Na Akakanusha Wanaoabudiwa Asiyekuwa Allaah Italindwa Mali Na Uhai Wake Na Hesabu Yake Itakuwa Kwa Allaah

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

05-Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akakanusha Wanaoabudiwa Asiyekuwa Allaah Italindwa Mali Yake Na Uhai Wake Na Hesabu Yake Itakuwa Kwa Allaah

 

 

 

عَنْ أَبِي مَالِكٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَكَفَرَ بِمَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللَّهِ حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ وَحِسَابُهُ عَلَى اللَّهِ)) مسلم‏

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Maalik kutoka kwa baba yake amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: ((Atakayesema “Laa ilaaha illa Allaah” na akakanusha wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai wake) na hesabu yake iko kwa Allaah)) [Muslim]

 

 

Share