Daraja Za Swalaah Zinatofuatiana Baina Ya Wanawake?

 

SWALI:

assalam alaikum warahmatulahi wabarakatuhu namshukuru mwanyezi mungu ambaye ametuwezesha kutupa uhai mpaka siku hii ili niweze kujielimisha na dini yetu, na rehma na amani zimfikie nabii wetu (swalalahu alaihi wasalama) ama baada ya salaam, swali langu ni hili lifwatao:

nilisikia eti ibada ya msichana alie olewa ibada yake in darja sabini kuliko idaba ya ule msichana hajaolewa ni kweli ao sio kweli? na kama ni kweli ningependea kuwa na ushahidi barakaLahu ghair wasalam alaikum warhamtulahi wa barakatu

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Hakuna tofauti yoyote baina ya Swalah ya msichana aliyeolewa na asiyeolewa. Wote thawabu zao ni sawa. Kusema kuwa aliyeolewa daraja yake ni sabiini kunahitajia dalili na hatukuona dalili inayotaja hivyo.   

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share