26-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah:Hakuna Anayeweza Kukizuia Alichokitoa Allaah Wala Kutoa Alichokizuia Wala Utajiri Wa Mtu Hautamsaidia Aliyetajiri Mbele Ya Allaah

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

 

26- Hakuna Anayeweza Kukizuia Alichokitoa Allaah Wala Kutoa Alichokizuia Wala Utajiri Wa Mtu Hautamsaidia Aliye Tajiri Mbele Ya Allaah

 

 

 عَنْ وَرَّادٍ، كَاتِبِ الْمُغِيرَةِ قَالَ: كَتَبَ مُعَاوِيَةُ إِلَى الْمُغِيرَةِ: اكْتُبْ إِلَىَّ مَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ فَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّ نَبِيَّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاَةٍ: (( لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهْوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ ‏))

Warraad (Mwandishi wa Al-Mughiyrah bin Shu'bah) amesema: Mu’aawiyah alimwandikia Al-Mughiyrah: Niandikie ambayo uliyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):  Basi akamwandikia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa akisema kila baada ya kumaliza Swalaah:  

 

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Allaahumma laa maani’a limaa A’-twayta, walaa mu’-twiya limaa mana’-ta, walaa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.  Ee Allaah, hakuna mwenye kukizuia Ulichokitoa, wala mwenye kutoa Ulichokizuia, na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako. [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

Tanbihi: Hii ni mojawapo wa Adhkaar za kila baada ya Swalaah.

 

 

Share