03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Hajj: Mlango Wa Adabu Na Sifa Za Ihraam

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْحَجِّ

Kitabu Cha Hajj

 

بَابُ وُجُوهِ اَلْإِحْرَامِ وَصِفَتِهِ

03-Mlango Wa Adabu Na Sifa Za Ihraam

 

 

 

592.

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {خَرَجْنَا مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم عَامَ حَجَّةِ اَلْوَدَاعِ، فَمِنَّا مَنْ أَهَلَّ بِعُمْرَةٍ، وَمِنَّا مَنْ أَهَلَّ بِحَجٍّ وَعُمْرَةٍ، وَمِنَّا مَنْ أَهَلَّ بِحَجٍّ، وَأَهَلَّ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِالْحَجِّ، فَأَمَّا مَنْ أَهَلَّ بِعُمْرَةٍ فَحَلَّ، وَأَمَّا مَنْ أَهَلَّ بِحَجٍّ، أَوْ جَمَعَ اَلْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ فَلَمْ يَحِلُّوا حَتَّى كَانَ يَوْمَ اَلنَّحْرِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Tulitoka pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika mwaka wa Hijjah ya kuaga,[1] na wengine wetu wakatamka Talbiyah kwa ajili ya ‘Umrah, wengine kwa ajili ya Hijjah pamoja na ‘Umrah, na wengine kwa ajili ya Hijjah peke yake. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitamka Talbiyah kwa ajili ya Hijjah. Wale waliotamka kwa ajili ya ‘Umrah peke yake wakajitengua  Ihraam. Lakini wale waliotamka kwa ajili ya Hijjah peke yake au wale waliounganisha Hijjah na ‘Umrah hawakutengua Ihraam zao hadi siku ya kuchinja.”[2] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

[1] Zipo aina tatu za Ibaada ya Hijjah nazo ni: (a)Ifraad ambapo Haji anaingia katika hali ya Ihraam kwa nia ya kutekeleza Hijjah peke yake. (b) Tamattu’ ambapo Haji hingia katika hali ya Ihraam katika kituo cha Miyqaat kwa nia ya kutekeleza ‘Umrah na kisha atekeleze Twawaaf (kutufu) na Sa’y (kusai). Iwapo kamleta mnyama wa kafara, basi asiivue Ihraam yake; na akiwa hakuleta mnyama basi aivue Ihraam yake wakati huo. Zikianza siku za Hijjah, lazima aingie katika hali ya Ihraam tena na aitekeleze Hijjah. (c) Qiraan ambapo Haji huingia katika hali ya Ihraam kwa nia ya kutekeleza ‘Umrah na Hijjah kwa pamoja. Wakazi wa Makkah hawaruhusiwi kutekeleza au kufanya Tamattu’ na Qiraan.

 

[2] Yawm An-Nahr ni siku ya kuchinja mnyama wa kafara, yaani tarehe 10 mwezi wa Dhul-Hijjah.

Share