Imaam Ibn Al-Qayyim:Tawassul Kwa Suwrah Al-Faatihah Imejumuisha Aina Tatu Za Tawhiyd

Tawassul Kwa Suwrah Al-Faatihah Imejumuisha Aina Tatu Za Tawhiyd

 

Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“(Suwrah hii) imejumuisha baina Tawassul kwa Allaah (Ta’aalaa) kwa himdi na thanaa (kumsifu na kumtukuza kwa wingi) na kumuadhimisha, na kutawassal Kwake kwa kumfanyia Yeye ‘ibaadah na Tawhiyd (kumpwekesha Kwake). Kisha likaja ombi muhimu kabisa la kuombwa na la tamanio la kufaulu kabisa nalo ni hidaaya baada ya wasiylah mbili. Basi mwombaji kwayo ana uhakika wa wa kuitikiwa” [Madaarij As-Saalikiyn (1/24)]

 

Amesema pia:

“Juu ya ufupi wake lakini inabeba aina zote tatu za Tawhiyd; Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola), Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (kumpwekesha Allaah katika ‘ibaadah), na Tawhiyd Al-Asmaa Wasw-Swifaat (Kumpwekesha Allaah katika Majina Na Sifa Zake).”

 

 

[Madaarij As-Saalikiyn (1/24-27)]

 

 

Share