Visheti Vya Kukandiwa Siagi Vya Kastadi

Visheti Vya Kukandiwa Siagi Vya Kastadi

 

Vipimo

 

Unga -  4 Vikombe vya chai

Siagi - 1 Kikombe cha chai

Kastadi (Custard)  vijiko vya supu

Hiliki   ½ Kijiko cha chai

 

Shira: 

 

Sukari - 2 Vikombe vya chai

Maji   - 1 Kikombe cha chai

Vanilla  ½ Kijiko cha chai

 

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi, kastadi na hiliki.
  2. Changanya vizuri isiwe na madonge.
  3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
  4. Halafu utakatakata vidoge vidogo design upendayo
  5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto  usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya brown light,  kisha viepue vichuje mafuta. .
  6. Changanya visheti na shira uchaganye vizuri.
  7. Vimwage katika sinia vipoe vikiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

 

 

 

Share