06-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Kufilisiwa Na Kuzuwia (Kutumia Mali)

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَلتَّفْلِيسِ وَالْحَجْرِ

06-Mlango Wa Kufilisiwa Na Kuzuwia (Kutumia Mali)

 

 

 

 

727.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ   قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَقُولُ: {مَنْ أَدْرَكَ مَالَهُ بِعَيْنِهِ عِنْدَ رَجُلٍ قَدْ أَفْلَسَ، فَهُوَ أَحَقُّ بِهِ مِنْ غَيْرِهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَرَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَمَالِكٌ: مِنْ رِوَايَةِ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ مُرْسَلًا بِلَفْظِ: {أَيُّمَا رَجُلٌ بَاعَ مَتَاعًا فَأَفْلَسَ اَلَّذِي اِبْتَاعَهُ، وَلَمْ يَقْبِضِ اَلَّذِي بَاعَهُ مِنْ ثَمَنِهِ شَيْئًا ، فَوَجَدَ مَتَاعَهُ بِعَيْنِهِ، فَهُوَ أَحَقُّ بِهِ، وَإِنْ مَاتَ اَلْمُشْتَرِي فَصَاحِبُ اَلْمَتَاعِ أُسْوَةُ اَلْغُرَمَاءِ} وَوَصَلَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ، وَضَعَّفَهُ تَبَعًا لِأَبِي دَاوُدَ 

وَرَوَى أَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ: مِنْ رِوَايَةِ عُمَرَ بْنِ خَلْدَةَ قَالَ: أَتَيْنَا أَبَا هُرَيْرَةَ فِي صَاحِبٍ لَنَا قَدْ أَفْلَسَ، فَقَالَ: لَأَقْضِيَنَّ فِيكُمْ بِقَضَاءِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَنْ أَفْلَسَ أَوْ مَاتَ فَوَجَدَ رَجُلٌ مَتَاعَهُ بِعَيْنِهِ فَهُوَ أَحَقُّ بِهِ} وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَضَعَّفَ أَبُو دَاوُدَ هَذِهِ اَلزِّيَادَةَ فِي ذِكْرِ اَلْمَوْتِ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Tulimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Atakayekuta mali yake ile ile kwa mtu aliefilisika, basi yeye ana haki zaidi[1] kuliko mwingine.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Abuu Daawuwd na Maalik wameipokea kwa Riwaayah ya Abuu Bakr bin ‘Abdir-Rahmaan[2][3] ikiwa ni Mursal kwa tamshi: “Yeyote mwenye kuuza bidhaa mwenye kuinunua akafilisika wala hakumlipa chochote katika thamani yake akaikuta bidhaa yake ile ile kama ilivyo, basi yeye ana haki zaidi kuichukua. Mnunuzi akifa, mwenye bidhaa akakuta mali yake kwake ana haki zaidi ya kuichukua.”[4] [Al-Bayhaqiyy ameidhoofisha akifuata Abuu Daawuwd]

 

Abuu Daawuwd na Ibn Maajah wameipokea kutoka katika Riwaayah ya ‘Umar bin Khaldah[5] amesema: Tulimuendea Abuu Hurayrah tukiwa na sahibu yetu aliyefilisika, akasema kwa hakika nitawahukumu kwa hukumu ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kufilisika au akafa, mtu akakuta mali yake ile ile basi yeye ana haki zaidi kwa mali hiyo.”[6] Ameisahihisha Al-Haakim. Abuu Daawuwd ameidhoofisha vile akaidhoofisha ziada hii inayoeleza kifo.

 

 

 

728.

وَعَنْ عَمْرِو بْنِ اَلشَّرِيدِ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَيُّ اَلْوَاجِدِ يُحِلُّ عِرْضَهُ وَعُقُوبَتَهُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَعَلَّقَهُ اَلْبُخَارِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

 Kutoka kwa ‘Amr bin Ash-Shariyd[7] kutoka kwa baba yake[8] amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tajiri kuzuia haki inayofaa kutolewa inamhalalishia kuharibiwa jina na kuadhibiwa[9].”[10] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaai na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

729.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {أُصِيبَ رَجُلٌ فِي عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فِي ثِمَارٍ اِبْتَاعَهَا، فَكَثُرَ دَيْنُهُ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  " تَصَدَّقُوا عَلَيْهِ" فَتَصَدَّقَ اَلنَّاسُ عَلَيْهِ، وَلَمْ يَبْلُغْ ذَلِكَ وَفَاءَ دَيْنِهِ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  لِغُرَمَائِهِ: " خُذُوا مَا وَجَدْتُمْ، وَلَيْسَ لَكُمْ إِلَّا ذَلِكَ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mtu mmoja katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipata hasara katika matunda aliyonunua, deni lake likazidi, akafilisika. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Mpeni Swadaqah, haikufikia kiasi cha kulipa deni analodaiwa. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaambia wanaomdai: “Chukueni mlichopata, hamna isipokuwa hicho tu.”[11] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

730.

وَعَنِ اِبْنِ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ، عَنْ أَبِيهِ، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ حَجَرَ عَلَى مُعَاذٍ مَالَهُ، وَبَاعَهُ فِي دَيْنٍ كَانَ عَلَيْهِ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَأَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ مُرْسَلًا، وَرُجِّحَ

Kutoka kwa Ibn Ka’b bin Maalik[12] amehadithia kutoka kwa baba yake[13] kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alizuia mali ya Mu’aadh akaiuza kulipa deni analodaiwa.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy, na akaisahihisha Al-Haakim. Abuu Daawuwd ameipokea ikiwa ni Mursal na kuipa nguvu]

 

 

 

731.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {عُرِضْتُ عَلَى اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَوْمَ أُحُدٍ، وَأَنَا اِبْنُ أَرْبَعَ عَشْرَةَ سَنَةً، فَلَمْ يُجِزْنِي، وَعُرِضْتُ عَلَيْهِ يَوْمَ اَلْخَنْدَقِ، وَأَنَا اِبْنُ خَمْسَ عَشْرَةَ سَنَةً، فَأَجَازَنِي} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبَيْهَقِيِّ: "فَلَمْ يُجِزْنِي، وَلَمْ يَرَنِي بَلَغْتُ". وَصَحَّحَهَا اِبْنُ خُزَيْمَةَ

 Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nilipitishwa kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) siku ya vita vya Uhud[14] nami ni mvulana wa umri wa miaka kumi na nne hakuniidhinisha. Nikapitishwa kwake siku ya vita vya Khandaq nami ni mvulana wa miaka kumi na tano akaniidhinisha.”[15] [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah nyingine ya Al-Bayhaqiyy: “…hakuniidhinisha wala hakuniona kuwa nimebaleghe.” Ameisahihisha Ibn Khuzaymah

 

 

 

732.

وَعَنْ عَطِيَّةَ اَلْقُرَظِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {عُرِضْنَا عَلَى اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَوْمَ قُرَيْظَةَ، فَكَانَ مَنْ أَنْبَتَ قُتِلَ، وَمَنْ لَمْ يُنْبِتْ خُلِّيَ سَبِيلُهُ، فَكُنْتُ فِيمَنْ لَمْ يُنْبِتْ فَخُلِّيَ سَبِيلِي} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ 

Kutoka kwa ‘Atwiyyah Al-Quradhwiyy[16] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulipitishwa kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) siku ya vita vya Quraydhwa, anauwawa aliyeota nywele (za kinena) na ambaye hajaota nywele anaachwa, mimi nilikuwa miongoni mwa ambao hawakuota nywele akaniacha.”[17] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]

 

 

 

733.

وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {لَا يَجُوزُ لِاِمْرَأَةٍ عَطِيَّةٌ إِلَّا بِإِذْنِ زَوْجِهَا}

وَفِي لَفْظٍ:{لَا يَجُوزُ لِلْمَرْأَةِ أَمْرٌ فِي مَالِهَا، إِذَا مَلَكَ زَوْجُهَا عِصْمَتَهَا} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَصْحَابُ اَلسُّنَنِ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

 Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb amepokea kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Haifai mwanamke kutoa kitu isipokuwa kwa idhini ya mumewe.”

Katika tamshi lingine: “Haifai mwanamke kufanya lolote katika mali yake[18] endapo mumewe amemiliki hifadhi yake.”[19] [Imetolewa na Ahmad na Maimaam wa Sunan[20] isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

734.

وَعَنْ قَبِيصَةَ بْنِ مُخَارِقٍ اَلْهِلَالِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {إِنَّ اَلْمَسْأَلَةَ لَا تَحِلُّ إِلَّا لِأَحَدِ ثَلَاثَةٍ: رَجُلٍ تَحَمَّلَ حَمَالَةً فَحَلَّتْ لَهُ اَلْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَهَا ثُمَّ يُمْسِكَ، وَرَجُلٍ أَصَابَتْهُ جَائِحَةٌ اِجْتَاحَتْ مَالَهُ، فَحَلَّتْ لَهُ اَلْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَ قِوَامًا مِنْ عَيْشٍ، وَرَجُلٍ أَصَابَتْهُ فَاقَةٌ حَتَّى يَقُولَ ثَلَاثَةٌ مِنْ ذَوِي الْحِجَى مِنْ قَوْمِهِ: لَقَدْ أَصَابَتْ فُلَانًا فَاقَةٌ، فَحَلَّتْ لَهُ اَلْمَسْأَلَةُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Qabiyswah bin Mukhaariq Al-Hilaaliyy[21] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika kuomba si halali kwa yeyote ila kwa moja ya mambo matatu: mtu aliyechukua dhamana, hapo ni halali kwake kuomba mpaka apate kisha atajizuia, mtu iliyoangamia mali yake, ni halali kwake kuomba mpaka apate msimamo wa maisha, na mtu aliyepata na uhitaji kwa umaskini hadi watu watatu wenye busara katika jamaa zake waseme: Hakika fulani amepata umaskini. Ni halali kwake kuomba.”[22] [Imetolewa na Muslim]

 


 

[1] Hii ina maana kuwa muuzaji anaweza kuvunja mkataba na mnunuzi na kuchukuwa mali yake ikiwa mnunuzi amefilisika.

 

[2] Huyu ni Abuu Bakr bin ‘Abdir-Rahmaan bin Al-Haarith bin Al-Mughiyrah Al-Makhzuwm Al-Madaniy, alikuwa ni kadhi wa Madiynah. Inasemekana kuwa jina lake lilikuwa Muhammad Al-Mughiyrah au Abuu Bakr, kun-ya yake ilikuwa ni Abuu Abdir-Rahmaan. Inasemwa hali kadhalika kuwa jina lake na kun-ya yake ilikuwa sawa. Alikuwa mtu madhubuti, Mwanazuoni na mwenye taqwa. Alikuwa ni Taabi’i wa kizazi cha tatu alifariki katika ukhalifa wa Al-Waliyd bin ‘Abdil Maalik.

 

 

[3] Abuu Bakr bin ‘Abdir-Rahmaan bin Al-Haarith Al-Makhzuwm Al-Madani. Ni madhubuti, faqihi, mfanya ‘ibaadah. Alifariki mwaka wa 94 Hijriyyah.

 

[4] Yaani atachukua kama wale wengine wanavyochukua kulingana na mafungu yao.

 

[5] Huyu ni Abuu Hafsi Al-Answaar Al-Madaniy Al-Qaadhwi. Alikuwa ni mtu mwenye heshima kubwa, mkali, mwenye taqwa na mtu mwenye kutegemewa. Amepokea kutoka kwa Abuu Hurayrah na Rabiy’a Ar-Raay amepokea kutoka kwake. Inasemekana kuwa Khaldah alikuwa ni babu yake na jina la babake lilikuwa ni ‘Abdur-Rahmaan.

 

[6] Ikiwa mnunuzi atafilisika baada ya kulipa kiwango cha fedha, muuzaji hana haki ya mali yote. Atachukua hisa ya mali yake tu. Mdaiwa akifa watapewa mali zao bila kujali ni mali ya nani iliyouzwa na ya nani haikuuzwa.

 

[7] Huyu ni Abul-Waliyd ‘Amr bin Ash-Shariyd bin Suwayd At-Thaqaaf At-Twaaif. Ni madhubuti. Abuu Ash-Shariyd ni Swahaba aliyehudhuria Bay’at Ar-Ridhwaan. Alikuwa ni Taabi’i wa kizazi cha tatu.

 

[8] Huyu ni Shariyd Suwayd Ath-Thaqaaf. Jina lake ni Maalik, lakini Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akampa jina Shariyd (aliyetoroka) baada ya kuwa mmoja wa watu wa ukoo wake, alikimbia hadi Makkah na akasilimu. Inasemekana asili yake ni kutoka Hadhramout, ila alijulikana ni wa ukoo wa Banuu Thaqif yaani watu wa Twaaif.

 

[9] Ikiwa mdaiwa ana uwezo wa kulipa deni kisha asilipe kwa makusudi, kwa hali hiyo mkopeshaji ana haki ya kumfedhehesha kwa kumkashifu mbele ya kadamnasi na kisha kumfungulia mashtaka.

 

[10] Kumkashifu ni kusema: “Fulani amezuwia haki yangu.” Na kumuadhibu ni kumfunga.

 

[11] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anakusudia kuwa hizi ni zote zilizokuwepo. Hivyo, aliwataka wadai kugawa alichomiliki sawa kwa sawa.

 

[12] Abuu Al-Khatwaab ‘Abdir-Rahmaan bin Ka’b bin Maalik Al-Answaar Al-Madaniy, alikuwa madhubuti na ni miongoni mwa taabi’iyna wakubwa. Inasemekana alizaliwa wakati wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na alikuwa wakati wa Khalifa Sulaymaan bin ‘Abdil-Maalik.

 

[13] Ka’b bin Maalik bin Abuu Ka’b Al-Answaar As-Sulami Al-Madaniy mshairi, alikuwa ni mmoja wa washairi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alihudhuria Bay’atul ‘Aqaba ya pili na vita vyote isipokuwa Badr na Tabuwk. Alikuwa mmoja miongoni  mwa watatu ambao toba yao ilitajwa katika Suwrat At-Tawbah kwa kubaki Madiynah wakati wa vita vya Tabuwk. Inasemekana kuwa alikufa baada ya kupofuka mwaka 50 au 51 Hijriyyah akiwa na umri wa miaka 77.

 

[14] Siku ya Uhud alikuenda kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuomba ruhusa kupigana katika vita vya Uhud dhidi ya makafiri wa Makkah.

 

[15] Sababu ya Hadiyth hii kuwekwa hapa ni kuonesha kuwa umri wa kukalifishwa mambo ni umri wa miaka 15 na maamrisho yote ya kishariy’ah yanakuwa wajibu wakati huo. Hivyo basi ambaye hajafikia umri huu muamala wake haukubaliki kama vile kuuza, kununua n.k. isipokuwa kwa ridhaa ya wazazi wake au aliyeteuliwa kuwa msimamizi wake atazuiwa yote hayo mpaka atakapo baleghe. Vivyo hivyo jambo linguine linalotibitisha kukua kwake na kuwajibika ni kuota kwa nywele za kinenani.

 

[16] ‘Atwiyyah Al-Quradhwiyy ni Swahaba mdogo aliyeripoti Hadiyth moja tu. Huyu ni kutoka katika kabila la Baniy Quraydhwa. Yasemekana kuwa aliishi Al-Kufah (‘Iraaq). Ibnu ‘Abdil-Barr amesema sikuweza kujua jina la baba yake. Mujaahid na wengineo wamepokea kutoka kwake.

 

[17] Hadiyth hii ni dalili kuwa anayemea nywele za sehemu ya siri huwa amebaleghe, yaani huchukuliwa kuwa ni mtu mzima anapitishwa hukmu zote.

 

[18] Mwanamke ana haki zote na mali zake bila ya ruhusa ya mumewe. Mali yake ni nini? Mahari yake, alichorithi, faida za biashara zake anazofanya mwenyewe, hizi ni mali za mke na mume hana mamlaka ya aina yoyote ile kwa mali hii. Mwanamke anaweza kumpa mumewe chochote anachotaka kumpa, na ni halali kwa mumewe. Kisa cha ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na mkewe kimetajwa huko nyuma, jambo hili lisingetokea kama mke hana haki katika mali yake.

 

[19] Al-Khattabi amesema: “Hadiyth hii inahimiza uhusiano bora baina ya mtu na mkewe au kwa mke ambaye akili yake haijakaa sawa, kwani imethubutu kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaambia wanawake: Toeni Swadaqah na wanawake wakatoa vipuli, mikufu n.k.”

 

[20] Yaani walioandika vitabu vya Sunan nao ni : At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, An-Nasaai na Ibn Maajah. Vitabu vyao ni Sunan At-Tirmidhiy, Sunan Abiy Daawuwd, Sunan An-Nasaai na Sunan Ibn Maajah.

 

[21] Qabiyswah bin Mukhaariq bin ‘Abdillaah bin Shaddaads Al-‘Amiri. Ni Swahaba. Alimtembelea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasilimu. Katika vitabu vya Hadiyth, ana Hadiyth sita. Aliishi Al-Basra (‘Iraaq).

 

[22] Hadiyth ikamalizikia hivi: “Kuomba kusiko tokana na sababu hizo ni haraam ee Qabiyswa, anayekula anakula haraam.”

 

 

Share