44-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Wasiya Wa Nabiy Nuwh: Laa Ilaaha Illa-Allaah Ni Nzito Katika Mizani Kuliko Mbingu Saba Na Ardhi Saba

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

 

44-Wasiya Wa Nabiy Nuwh:

Laa Ilaaha Illa-Allaah Ni Nzito Katika Mizani Kuliko Mbingu Saba Na Ardhi Saba

 

 

عن عبد الله بن عمرو: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ نبيَّ اللهِ نوحًا لما حضَرَتْه الوفاةُ قال لابنِه: إني قاصٌّ عليك الوصيَّةَ، آمرُك باثنتَينِ و أنهاك عن اثنتَينِ، آمرُك ب ( لاإله إلا اللهُ )، فإنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضينَ السبعَ لو وُضِعَتْ في كِفَّةٍ، ووُضِعَتْ لا إلهَ إلا اللهُ في كِفَّةٍ، رجَحَتْ بهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ، ولو أنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضَينَ السبعَ كُنَّ حَلْقةً مُبهَمةً قصَمَتْهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ، وسبحانَ اللهِ وبحمدِه فإنها صلاةُ كلِّ شيءٍ، وبها يُرزَقُ الخلقُ، و أنهاك عن الشركِ و الكِبر))ِ قال: قلتُ: أوْ قيل: يا رسولَ اللهِ هذا الشركُ قد عرفْناه فما الكِبْرُ؟  قال: أن يكون لأَحدِنا نعْلانِ حسَنتانِ لهما شِراكانِ حسنانِ؟ قال: ((لا)) قال: هو أن يكون لأحدِنا أصحابٌ يجلسون إليه؟ قال: ((لا)) قيل: يا رسولَ اللهِ فما الكِبْرُ؟ قال: ((سَفَهُ الحقِّ و غَمْصُ الناسِ)) السلسلة الصحيحة 134

 

Mauti yalipomfikia Nabiy wa Allaah (ambaye ni) Nuwh (‘Alayhis-Salaam) alimwambia mwanawe: Nakuhadithia wasiya wangu;  Nakuamrisha mambo mawili na kukukataza mawili.  Nakuamrisha Laa ilaaha illa Allaah (Hapana mwabudiwa wa haki illa Allaah) kwani ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimewekwa katika mizani na Laa ilaaha illa Allaah imewekwa katika mizani ya pili basi  Laa ilaaha illa Allaah ingelikuwa nzito.

 

Na kama ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimefungwa katika mduara,  basi  Laa illa Allaah ingelivunja mduara huo.

 

La pili nakuamrisha Subhaana-Allaahi wa Bihamdihi (Ametakasika Allaah kwa Himdi Zake) kwani ni du'aa ya kila kitu na kwayo viumbe wanaruzukiwa.

 

Na nakukataza shirki  na kiburi. (Msimuliaji akasema: Nikauliza au mtu akauliza) “Ee Rasuli wa Allaah! Shirki tunaifahamu, lakini je, nini kiburi? Je, ni vile mmoja wetu kuwa na viatu vyenye utepe mzuri?”

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hapana!))

 

Akauliza tena:  Je, (kiburi ina maana) ni vile mmoja wetu kuwa ana marafiki wanaoketi naye?

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hapana!))

 

Mtu akauliza:  Ee Rasuli wa Allaah! Basi ni nini kiburi?

 

Akasema: ((Ni  kukataa haki na kudharau watu)) [As-Silsilah Asw-Swahiyhah (134)]

 
 
Share